KWA SIMBA HII YA MGUNDA TUNAMFUNGA AL AHLY NNJE NDANI...UBINGWA UKO WAZI KWETU


Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo 


Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amefunguka mara baada ya kushinda bao 3-0 mchezo wao wa Ligi dhidi ya Azam FC na kusema bado wanaitafuta nafasi ya kwanza.
 
Katika msimamo wa Ligi, Yanga wanaongoza wakiwa na alama 68 katika michezo 25, Azam nafasi ya pili alama 57 na michezo 26 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu na alama 57.
 
“Bado alama moja na safari yetu bado inaendelea, tunaitafuta nafasi ya kwanza. Kwa mujibu wa gepu lililopo, nafasi bado tunayo, sisi hatutafuti nafasi ya pili. Ikitokea tumekwama tukaangukia nafasi ya pili basi hakuna mashaka lakini malengo yetu nasema leo hii ni kuitafuta nafasi ya kwanza.
 
“Kwa ubora tulionao, tunaiona nafasi ya kwanza inanukia na sisi Simba hatukati tamaa mpaka nafasi ya mwisho. Nilisema Simba itapiganiwa na ambao wana moyo wa kuipigania Simba sio wa kukata tamaa. Kwa wakati ambao watu wanatukatia tamaa, Simba inaanza kushinda mechi zote.
 
“Tunachokitaka ni kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kushiriki Kombe la Shirikisho ni kujidhulumu nafsi zetu na Simba yenyewe, hatuko tayari kwa hilo,” amesema Ahmed.
 
Mchezo unaofuata wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa timu ya Simba Sc ni dhidi ya Kagera Sugar FC unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili ya Mei 12, 2024.
 
Katika Hatua nyingine, Ahmed Ally amesema kuwa wanatamani kurudiana na timu zote walizocheza nazo msimu huu zikawafunga.
 
Ahmed amesema hayo mara baada ya Simba kuichapa Azam FC mabao 3-0 mchezo wao wa Ligi uliopigwa katika Dimba la Mkapa na kuongeza kuwa, Simba sasa imeimarika na kurejesha makali yake.
 
“Hii ni salam kwa yeyote anayekuja, Simba imeshika moto. Tunatamani wale wote ambao tumecheza nao kama kuna nafasi ya kurudiana nao muda huu, Simba SC tupo tayari. Simba hii kama tunapewa Al Ahly turudiane nao Ligi ya Mabingwa Afrika, anakufa nyumbani na ugenini, hilo wala halina mashaka.
 
“Hawezi kukukosa Chasambi, Karabaka au Balua, ngoma ikiwa ngumu atakufunga hata kocha. Mtazame Fredy alivyokuwa anawapeleka moto mabeki wa Azam FC. Simba sasa ipo sawa sawa, yeyote anayetaka aje,” amesema Ahmed Ally.

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 05/21/2024