Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo
KLABU ya
Simba iko mbioni kuhakikisha wanampa mkataba mpya kipa wao, Ayoub Lakred kusalia ndani ya timu hiyo kwa msimu ujao aa mashindano Imeelezwa.
Kulikuwa na taarifa kuwa nyota huyo huenda akaondoka ndani ya klabu hiyo baada ya mkataba wake kufikia ukingoni mwa msimu huu baada ya kusaini mwaka mmoja.
Mbali na kipa huyo lakini pia wamemueweke ofa kiungo Clatous Chama kama ataridhika na alichowekewa mezani asaini mkataba mpya kusalia ndani ya kikosi cha timu hiyo.
Taarifa za uhakika zilizotufikia ni kuwa baadhi ya wachezaji mikataba yao imefikia ukingoni akiwemo Kipa (Ayoub) ambaye ameridhia kuendelea kusalia ndani ya Simba na kuongeza mkataba.
Mtoa habari huyo amesema Chama na Kibu (Dennis) wamewekewa ofa mezani na kilichokuwepo wao kukubaliana na kilichopo mezani na kusainia mkataba.
"Kuna asilimia kubwa ya Ayoub kusalia ndani ya Simba kwa sababu mazungumza ya kuendelea kuitumikia timu kwa msimu ujao upo na kabla ya kuondoka baada ya kumalizika kwa ligi atasaini mkataba mwingine," amesema mtoa habari huyo.
Alipotafutwa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema mambo mazuri yanakuja na wachezaji mikataba yao iliyofikia ukingoni wanaohitajika wataendelea kusalia ndani ya kikosi.
"Hakuna mchezaji ambaye yupo kikosi cha kwanza na amefanya vizuri ndani ya timu kama ilivyo kwa kipa wetu ataondoka, niwahakikishie mashabiki na wanasimba kuwa wachezaji muhimu wote wataongezewa mkataba na kuleta wengine wapya," amesema Ahmed.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.