UCL - Real Madrid v Manchester City 


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 UEFA Champions League 

Semi-Final - First-Leg 

Real Madrid v Manchester City 

Estadio Santiago Bernabeu 
Madrid, Spain
Tuesday, 9 May 2023 
Kick-Off is at 21h00  
 
Manchester City watakuwa mgeni wa Real Madrid kwenye mechi ya klabu bingwa ulaya (UEFA) Mei 9 ugani Estadio Santiago Bernabeu.
 
Matokeo ya hivi karibuni katika shindano hili.
 
Mabingwa hao wa England walifuzu kuingia semi fainali baada ya kuishinda Bayern Munich ya Ujerumani kwa jumla ya mabao manne kwa moja hatua ya robo fainali. 
 
City hawajapoteza mechi ya UEFA katika michezo kumi iliyopita huku wakiandikisha ushindi wa mechi sita na kupata sare nne. 
 
Vile vile, the Citizens hawajapoteza mechi hata moja ya shindano hili katika michezo mitano iliyopita wakiwa nyumbani baada ya kushinda mechi nne mfululizo na kupata sare moja. 
 
Vikosi.
 
Kwa sasa the Citizens hawana mchezaji anayetumikia adhabu au marufuku ila wanafuatilia hali ya Kevin De Bruyne baada ya kukosa mechi ya Jumatano dhidi ya West Ham United kutokana na jeraha. 
 
Mlinzi Benjamin Mendy raia wa Ufaransa alisimamishwa na klabu hiyo baada ya kukabiliwa na madai ya ubakaji. 
 
Wachezaji muhimu
 
City wataweka matumaini yao kwa mshambuliaji mahiri Erling Haaland raia wa Norway anayeongoza chati ya wafungaji bora wa shindano hili msimu huu akiwa na magoli 12. Sio Haaland tu, kiungo Riyad Mahrez amefanikiwa kufunga magoli matatu na kusaidia mengine mawili msimu hivyo basi anatarajiwa kuipa taabu sana safu ya ulinzi ya Madrid. 

Erling Haaland
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Nukuu
 
“Nadhani timu zote ulimwenguni zinaamini kuwa ili kushinda shindano hili sharti uwaondoe Madrid,” alisema meneja wa City Pep Guardiola. 
 
“Zamani ilikuwa Barcelona ila wakati huu ni Madrid. Nafurahi kufika hatua ya nusu fainali ya shindano hili kwa miaka mitatu mfululizo. 
 
"Ushindi wa 4-1 kwa ujumla sio kiashiria cha hali halisi ya mchezo. Madrid wanatumia nguvu sana, wanajituma sana na wanayo maarifa. Wananifurahisha wanavyocheza. Shindano hili ni sharti uzingatie mbinu kwa kina.” 
 

Takwimu baina ya timu hizi.

 
Madrid na City wamekutana mara nane katika shindano hili la UEFA.
 
Wameshinda mara tatu kila mmoja na mechi mbili kuishia sare. 
 
Ratiba ya mechi za UEFA nusu fainali. 
 

Majira ya Afrika ya Kati. 

 
Tuesday, Mei 9 Jumanne
 
9:00pm - Real Madrid v Manchester City
 
Mei 10 Jumatano.
 
9:00pm - AC Milan v Inter Milan

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 05/09/2023