Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 UEFA Champions League
Semi-finals
Second leg
Manchester City v Real Madrid
Etihad Stadium
Manchester, England
Wednesday, 17 May 2023
Kick-off is at 21h00
Manchester City wapo mbioni kufika fainali ya mashindano ya klabu bingwa barani ulaya na watakuwa mwenyeji wa Real Madrid Etihad Stadium kwenye
mechi ya mkondo wa pili Jumatano Mei 17.
The Citizens walilazimisha sare ya 1-1 dhidi ya mabingwa watetezi kwenye mechi ya mkondo wa kwanza iliyochezwa Jumanne Mei 9 baada ya Kevin De Bruyne kufunga goli dakika ya 67 na kusawazisha goli la awali dakika ya 36 la Vinicius Junior.
Matakeo hayo yatawapa matumaini makubwa Manchester City kufika fainali ya shindano hili kwa mara ya pili katika historia ya klabu hiyo.
City walipata ushindi wa 4-3 nyumbani dhidi ya Madrid katika mechi ya kusisimua ya nusu fainali msimu 2021-22 kabla ya kuondolewa na Madrid kwenye mechi ya marudiano ambapo mchezo uliisha 3-1 katika muda wa ziada.
City ambao ni mabingwa wa ligi ya England hawajapoteza mechi ya UEFA msimu huu wakiwa nyumbani. Wameshinda mechi zote tano wakiwa nyumbani huku wakifanikiwa kufunga magoli 20 na kuruhusu magoli 2 tu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
De Bruyne amekuwa na mchango mkubwa katika timu yake kwenye shindano hili huku akichangia magoli mengi na kufunga vile vile. Alichangia magoli 4 hatua ya muondoano, alifunga goli 1 na kusaidia goli moja kwenye ushindi wa 7-0 dhidi ya RB Leipzig mechi ya 16 bora mkondo wa pili na kisha kusaidia goli la Erling Haaland dhidi ya Bayern Munich mechi ya mkondo wa pili ya robo fainali. De Bruyne alifunga goli zuri sana la kusawazisha dhidi ya Madrid vile vile kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali.
Katika habari za vikosi, Guardiola ana kikosi kizima ukiachia mbali Nathan Ake ambaye yupo nje akiuguza jeraha la misuli. Madrid hawana majeruhi yeyote hivyo basi Carlo Ancelotti atakuwa na wachezaji wote kwenye mechi hiyo.
Guardiola alieleza kuwa mechi ya marudiano mjini Manchester itakuwa kama fainali na anatarajia kufanya mabadiliko madogo baada ya kukiri kuwa mbinu za mechi ya kwanza zilimpoteza Erling Haaland mchezoni.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Mechi ya nyumbani itakuwa kama fainali kwani tutakuwa na mashabiki wetu. Tunautazamia mchezo huo,” alisema Guardiola. “Tulijituma sana. Unaweza kulinganisha mchezo huu na mechi ya mchujo.”
"Tunaelewa mbinu zao. Pengine watafanya mabadiliko. Tunahitaji kuimarisha safu yetu ya ulinzi na ushambuliaji vile vile kwa sababu David Alaba na Antonio Rudiger walimbana sana Erling Haaland. Federico Valverde na Toni Kroos walidhibiti safu ya kati vizuri na kuzuia mpira kumfikia Erling.
"Tutafanya mabadiliko machache katika mechi ya marudiano ili kuimarisha mtiririko wetu kwa sababu tutakuwa nyumbani na mashabiki wetu watakuwa nyuma yetu. Tutajituma sana kwa sababu mshindi wa mechi hii atapata nafasi ya kufika fainali.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za UEFA.
Mechi - 5
Man City - 3
Real Madrid - 1
Sare - 1
Ratiba ya mechi za UEFA mkondo wa pili nusu fainali:
Mei 16 Jumanne
9:00pm: Inter Milan v AC Milan
Mei 17 Jumatano
9:00pm: Manchester City v Real Madrid
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.