Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 FA Cup
Final
Manchester City v Manchester United
Wembley Stadium
London, England
Saturday, 3 June 2023
Kick-off is at 17h00
Manchester City watamenyana na Manchester United katika mechi ya fainali ya
kombe la FA mnamo Juni 3 Jumamosi ugani Wembley.
The Citizens walitawazwa mabingwa wa ligi ya Premier kwa mara ya tatu mfululizo walipomaliza alama tano juu ya Arsenal wikendi iliyopita.
Vile vile, City chini ya Pep Guardiola walifuzu kucheza fainali ya klabu bingwa ulaya UEFA hivyo basi kuwa na fursa ya kushinda mataji matatu kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo watakapomenyana na Inter Milan Ataturk Olympic Stadium mjini Istanbul Juni 10.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
City hawajaruhusu goli lolote katika shindano hili msimu huu huku wakipata ushindi wa 4-0, 1-0, 3-0, 6-0 na 3-0 dhidi ya Chelsea, Arsenal, Bristol City, Burnley, na Sheffield United mtawalia katika safari yao kuelekea fainali.
Mara ya mwisho City walicheza fainali ya shindano hili mwaka 2019 dhidi ya Watford ambapo waliibuka na ushindi wa 6-0. Awali mwaka 2013, City walipoteza fainali ya FA 1-0 dhidi ya Wigan.
Riyad Mahrez amefunga magoli matano katika mechi tano msimu huu ikiwa ni pamoja na magoli matatu dhidi ya Sheffield United mkondo wa nusu fainali. Raia huyo wa Algeria alisaidia kupatikana kwa magoli 11 katika ligi na anatarajiwa kuchangia pakubwa dhidi ya Red Devils kwani inakisiwa Jack Grealish anaweza kukosa mechi hiyo kutokana na jeraha.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Grealish alikosa mechi ya mwisho ya msimu dhidi ya Brentford pamoja na wachezaji Manuel Akanji, Ruben Dias na Kevin De Bruyne huku Guardiola akikiri kuwa watatu hao wanauguza majeraha madogo na kuonyesha imani huenda wakashiriki mechi dhidi ya United.
"Kuna wachezaji wanne au watano wanaouguza majeraha madogo. Sio makubwa ila ni majeraha,” alisema raia huyo wa Uhispania. “Wachezaji ambao hawakushiriki mechi dhidi ya Brentford walikuwa na uchovu mwingi.
"Wachezaji waliobaki Manchester kama Ruben hajashiriki mazoezi kwa siku 10 kama ilivyo kwa Jack Grealish. Kevin hakujihisi vizuri baada ya mchezo dhidi ya Brighton. Hiyo ndio hali halisi.
"Sio tatizo kubwa. Nahisi watakuwa tayari. Nitaangalia hali yao katika mazoezi siku tatu zijazo. Lilikuwa jambo zuri kuwaona leo na kujua hali yao kiafya.
"Tutawachezesha wachezaji wasio na majeraha au maumivu katika fainali. Ilikuwa ni vizuri kuwapa muda wachezaji waliocheza leo ili kuwapa nafasi wengine kupumzika na kuuguza majeraha.
"Watashiriki mazoezi Jumatano na kupumzika. Namiini watakuwa wamepona ila kwa sasa sina uhakika.”
Takiwmu baina ya timu hizi:
Mechi - 189
Man City - 58
Man United - 78
Sare - 53
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.