EPL - Newcastle United v Arsenal


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 35

Newcastle United v Arsenal

St James' Park
Newcastle upon Tyne, England
Sunday, 7 May 2023
Kick-off is at 17h30 
 
Baada ya ushindi mmoja katika mechi tano, Arsenal watakuwa wageni wa Newcastle United kwenye mchezo wa ligi mnamo Mei 7 Jumapili ugani St James' Park.
 
The Gunners walipoteza 4-1 kwenye mechi yao na City uwanjani Etihad tarehe 26 Aprili, ikiwa ni mechi ya kwanza kupoteza tangu Februari 15 hivyo basi kupoteza nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza mwaka huu.
 
Japo kwa muda mfupi, vijana wa Mikel Arteta walikaa kileleni mwa jedwali baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Chelsea ugani Emirates Jumanne Mei 2 kwani City walirudi katika nafasi ya kwanza baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya West Ham Jumatano Mei 3.  
 
Arsenal wapo hatarini kukosa taji la ligi baada ya kutoa sare tatu mfululizo; Liverpool (2-2), West Ham (2-2) na Southampton (3-3) kabla ya mechi yao dhidi ya City, matokeo yaliyopelekea wapinzani wao wa karibu kukwea kileleni mwa ligi.

Callum Wilson
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Baada ya kushindwa 3-0 na Aston Villa, the Magpies wameshinda mechi tatu za ligi mfululizo na kuweka hai matumaini yao ya kumaliza nne bora.
 
Kwa sasa Newcastle wanashikilia nafasi ya tatu, alama mbili mbele ya United baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Southampton japokuwa wamecheza mechi moja zaidi.
 
Callum Wilson amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu hiyo kwani amefunga magoli nane katika mechi saba. Mara nyingi msimu huu Wilson ametumika kama mchezaji wa akiba kutokana na mshambuliaji mpya Alexander Isak kuonyesha uwezo mkubwa wa kufunga magoli ila amekumbatia nafasi kila anapopata na sasa ametikisa wav umara 15 msimu huu katika ligi.

Martin Odegaard
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Martin Odegaard alipewa kitambaa cha unahodha mwanzoni mwa msimu na amekuwa akicheza vizuri na kuisaidia Arsenal kuwa miongoni mwa timu zinazofukuzia ubingwa wa ligi. Raia huyo wa Norway alifunga mabao mawili dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa ligi uliopita. Hadi sasa amefikisha idadi ya mabao 14 katika mechi 33 msimu huu huku pia akisaida kupatikana kwa mabao 8.
 
Katika habari za vikosi, wenyeji Newcastle wanazidi kumkosa mchezaji Emil Krafth anayeuguza jeraha la goti. Huenda Allan Saint-Maximin anayesumbuliwa na jeraha la paja na Sean Longstaff anayeuguza kisigino wakahusika kwenye mechi hiyo. Takehiro Tomiyasu na Mohamed Elneny wanauguza jeraha la goti huku William Saliba akisumbuliwa na mgongo na wote wanatarajiwa kukosa mechi hiyo. Vile vile, haijabainika wazi iwapo Gabriel Magalhaes atashiriki mechi hiyo.
 
Kocha wa Newcastle Eddie Howe alisifia athari za faida za mchezaji Wilson kwenye mchezo dhidi ya Southampton alipofunga magoli mawili akitokea kwenye benchi kama mchezaji wa akiba.
 
"Alifunga mabao yake kwa ustadi. Alionyesha mchezo mzuri kwa ujumla. Alileta uhuiano kwenye timu na pia mashabiki. Isak alicheza vizuri sana akitokea pembezoni kushoto. Tulionyesha mchezo wa kufana sana kipindi cha pili ambapo Callum Wilson alifanikiwa kufunga mabao mawili,” alisema Howe.
 
Arteta anaamini kuwa wachezaji wake wamerudia hali yao ya awali baada ya msururu wa matokeo yasiyo ya kuridhisha kwani walifunga magoli matatu kipindi cha kwanza dhidi Chelsea.
 
"Timu hii imerudia hali yake ya awali. Wachezaji walijituma sana, walionyesha kasi na nia kwenye mchezo. Mashabiki wetu walitushabikia tangu dakika ya kwanza. Tulifunga magoli mawili mazuri na kudhibiti mchezo kikamilifu. Tulistahili kushinda mechi hiyo,” alisema raia huyo wa Uhispania.
 
"Tulikuwa na nia ya kuonyesha kwamba bado tunao uwezo. Tulijiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo. Tulikuwa katika hali nzuri kiakili kuelekea mchezo huo. Kila kitu kilienda vizuri kwa ujumla."
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Newcastle - 1
Arsenal - 3
Sare - 1
 

Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 35:

 
Mei 6 Jumamosi
 
5:00pm: Bournemouth v Chelsea
 
5:00pm: Manchester City v Leeds United
 
5:00pm: Tottenham Hotspur v Crystal Palace
 
5:00pm: Wolverhampton Wanderers v Aston Villa
 
7:30pm: Liverpool v Brentford

 
Mei 7 Jumapili
 
6:30pm: Newcastle United v Arsenal
 
9:00pm: West Ham United v Manchester United

 
Mei 8 Jumatatu
 
5:00pm: Fulham v Leicester City
 
7:30pm: Brighton & Hove Albion v Everton
 
10:00pm: Nottingham Forest v Southampton
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

 

Published: 05/05/2023