EPL - Manchester United v Fulham


Hakimiliki ya picha: Getty Images

2022/23 English Premier League

Matchday 38

Manchester United v Fulham

Old Trafford
Manchester, England
Sunday, 28 May 2023
Kick-off is at 17h30 CAT
 
Manchester United wanatazamia kuendeleza ubabe wao dhidi ya Fulham watakapokutana kwenye mechi ya ligi ya kumalizia msimu mnamo Jumapili Mei 28.
 
The Red Devils wamepoteza mechi tatu tu za ligi dhidi ya the Cottagers tangu mfumo mpya wa ligi ya Premier na hawajapoteza mechi ya ligi katika michezo 14 iliyopita dhidi yao huku wakiandikisha ushindi wa mechi 11 kati ya idadi hiyo
 
United chini ya Erik ten Hag waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Fulham kwenye mechi ya mkondo wa kwanza Novemba 13. The Red Devils walikuwa katika hatari ya kubanduliwa kutoka kombe la FA baada ya Aleksandar Mitrovic kufunga goli dakika tano kipindi cha pili kilipoanza ugani Old Trafford.
 
Hata hivyo, hali hiyo ilibadilika Willian alipoonyeshwa kadi nyekundu kwa kushika na kuzuia mkwaju wa Jadon Sancho kuingia wavuni. Kocha Marco Silva na mchezaji Mitrovic waliaga mechi hiyo mapema vile vile kwani walionyeshwa kadi nyekundu kwa kubishana na mwamuzi kuhusu uamuzi wa kumtimua Willian.  Bruno Fernandes alisawazisha kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 75 kabla ya Marcel Sabitzer kuongeza goli la pili dakika mbili baadaye. Nahodha wa siku Bruno Fernandes alifunga goli la tatu dakika za nyongeza na kuipa United ushindi mkubwa..
 
United na Newcastle wanashika nafasi ya tatu na alama 69 kwa pamoja huku Newcastle ikiwazidi kwa ubora wa magoli. Timu zote mbili zina alama tatu zaidi ya Liverpool.
 
Casemiro of Manchester United
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
Fulham walipata ushindi dhidi ya Leicester City na Southampton kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Crystal Palace Jumamosi iliyopita na kujihakikishia nafasi kumi bora.  
 
Ushindi wa 3-1 wa Brentford dhidi Tottenham uliwahakikishia kumaliza nafasi ya 9 katika jedwali.
 
Casemiro amekuwa na mchango mkubwa kwa timu ya United tangu alipojiunga nao akitokea Real Madrid mwezi Agosti. Raia huyu wa Brazil alifunga goli zuri sana dhidi ya the Cherries na kufikisha idadi ya magoli matatu katika michezo 26 aliyoshiriki.
 
Aleksandar Mitrovic of Fulham
 Hakimiliki ya picha: Getty Images

Mitrovic alifungiwa mechi 8 kutokana na kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchuano wa FA lakini alirudi kwa kishindo mapema mwezi huu. Mshambuliaji huyo raia wa Serbia alifunga goli dhidi ya Southampton na kufuatisha kwa kufunga magoli mawili dhidi ya Palace. Mchezaji huyo amefikisha idadi ya magoli 14 katika michezo 23.
 
Katika vikosi, Lisandro Martinez, Tom Hean, Donny van de Beek na Marcel Sabitzer watakosekana kwa upande wa United kutokana na majeraha tofauti ila Marcus Rashford anatarajiwa kurejea baada ya kuugua. Fulham watakosa huduma za Andreas Pereira, Tim Ream, Dan James na Layvin Kurzawa.
 
Ten Hag alisifia uchezaji wa Casemiro dhidi ya Bournemouth huku akikiri kuwa amefanya vizuri sana kuliko walivyotarajia tangu alipojiunga na timu hiyo.
 
"Anazidi kutushangaza kila uchao,” alisema Ten Hag."Ni mwanasoka mzuri. Anacheza kwa ajili ya timu. Anajituma na anajua kuchezesha timu. Ana uwezo mkubwa wa kufunga magoli pia.
 
"Amepita matarajio yetu. Tulikuwa tumekosa mchezaji wa safu ya kiungo. Tulimpata lakini haikuwa rahisi kwa kuwa hawatikani wachezaji sampli hiyo kwa urahisi hasa kwa viwango vya Manchester United. Tunafurahi sana kumpata.
 
"Amekuwa na mchango mkubwa na tulikosa huduma zake katika mechi nane au tisa alizotumikia adhabu. Hakuwepo mechi za kwanza za msimu lakini anapocheza timu huwa na mpangilio mzuri. Tumeshinda mechi nyingi anapocheza.”
 
Silva aliwapongeza wachezaji wake kwa juhudi zao msimu huu.
 
"Hakuna aliyetarajia sisi kuwa hapa tulipo sasa hivi,” alisema raia huyo wa Ureno. “Wengi walitabiri tutakuwa wa kwanza kushuka daraja na mengine mengi ambayo sitaki kurudia.
 
"Umekuwa msimu wa kufana kwetu. Wachezaji hawa wameonyesha juhudi kubwa kila siku. Wapo sawa kiakili kukabiliana na changamoto, kujifunza na kuimarika ambalo ni jambo muhimu. Nawapongeza sana.
 
"Bado safari haijakamilia. Juma lijalo tunaweza kuzungumza lakini ni vizuri kuwapongeza kwa yote waliyofanikisha msimu huu hadi kufikia sasa.”
 

Takwimu baina ya timu hizi mechi 5 za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Man United - 4
Fulham - 0
Sare - 1
 
Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 38:
 
Mei 28 Jumapili
 
5:30pm: Arsenal v Wolverhampton Wanderers
 
5:30pm: Aston Villa v Brighton & Hove Albion
 
5:30pm: Brentford v Manchester City
 
5:30pm: Chelsea v Newcastle United
 
5:30pm: Crystal Palace v Nottingham Forest
 
5:30pm: Everton v Bournemouth
 
5:30pm: Leeds United v Tottenham Hotspur
 
5:30pm: Leicester City v West Ham United
 
5:30pm: Manchester United v Fulham
 
5:30pm: Southampton v Liverpool

 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

 

Published: 05/26/2023