EPL - Manchester City v Chelsea


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 37

Manchester City v Chelsea

Etihad Stadium
Manchester, England
Sunday, 21 May 2023
Kick-off is at 18h00  
 
Manchester City watatawazwa mabingwa wa ligi ya Premier kwa mara ya tatu mfululizo iwapo wataibuka na ushindi dhidi ya Chelsea ugani Etihad Jumapili Mei 21.
 
The Citizens wanaongoza ligi kwa alama 4 baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Everton Goodison Park Jumapili iliyopita huku wapinzani wao wa karibu Arsenal wakipoteza 3-0 mikononi mwa Brighton uwanjani Emirates saa chache baadaye.
 
Timu ya Pep Guardiola ina mchezo mmoja mkononi hivyo basi wakipata ushindi dhidi ya Chelsea itakuwa ni vigumu kwa aliye nafasi ya pili kumfikia. Hii itawapelekea kutwaa taji hilo huku zikisalia mechi mbili msimu kukamilika.

Erling Haaland
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Chelsea chini ya Frank Lampard hawajafanya vizuri tangu kurejea kwake Aprili 6 na kuchukua mikoba ya Graham Potter.
 
Chelsea walilazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Nottingham Forest ugani Stamford Bridge Jumamosi iliyopita, baada ya Lampard kupata ushindi wake wa kwanza wa 3-1 dhidi ya Bournemouth wikendi ya awali Vitality Stadium.
 
Kuna uwezekano wa Chelsea kumaliza kumi bora ifikapo mwisho wa msimu lakini wanahitaji kushinda mechi zilizosalia kwani Fulham wanashika nafasi ya 10 alama nane mbele yao na mchezo mmoja zaidi.
 
Erling Haaland alifunga goli dhidi ya Toffees na kuongeza idadi yake hadi 36 kutokana na michezo 33. Hazijapita mechi mbili kwa raia huyo wa Norway bila kufunga goli na sasa anabakiza mabao manne tu kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya ligi ya Premier kufikisha magoli 40 msimu mmoja.

Raheem Sterling
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Raheem Sterling amekuwa na wakati mgumu kuonyesha uwezo uliofanya Chelsea kutumia fedha nyingi kumtoa City. Vile vile, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 amekumbwa na majeraha ya mara kwa mara. Baada ya mechi 11 bila kufunga goli, mchezaji alifanikiwa kufunga magoli mawili dhidi ya Everton.
 
Katika habari ya vikosi, Nathan Ake wa City anauguza jeraha la paja hivyo basi atakosa mechi hiyo.  Chelsea na Lampard watakosa huduma za wachezaji Armando Broja, Reece James, Marc Cucurella, Ben Chilwell, Kalidou Koulibaly, N'Golo Kante, Mason Mount, Marcus Bettinelli na Mateo Kovacic wanaoguza majeraha ya viungo tofauti tofauti.
 
Guardiola aliendelea kumsifu mchezaji Ilkay Gundogun baada ya kufunga magoli mawili dhidi ya Everton na kusaidia timu yake kushinda mechi ya 11 ya ligi mfululizo. Siku nane kabla, kiungo huyo alifunga magoli mawili dhidi ya Leeds.
 
"Kwa mara nyingine Ilkay anazidi kuonyesha uwezo wake na umuhimu wake na vile anavyojitolea kwa ajili ya timu na klabu,” alisema raia huyo wa Uhispania.
 
"Sio ufungaji wa magoli tu bali pia mwendelezo wa uchezaji mzuri. Dhidi ya Leeds alikuwa mchezaji bora wa timu yetu na leo vile vile ameonyesha tena. Anafanya kila kitu kwa weledi.
 
"Sio mzungumzaji sana ila inapozungumza kila mmoja anatega sikio. Ni kiongozi. Anadhihirisha kila wakati katika mazoezi. Anazingatia muda na anafurahia kazi yake.”  
 
Lampard alifurahi kuona Sterling akifunga magoli huku akikiri kuwa timu yake imekuwa ikikosa makali hasa kuelekea ukingoni mwa ligi.
 
"Raheem anaimarika hatua kwa hatua. Ni mfungaji mzuri mwenye uzoefu katika ligi ya premier na taifa lake,” alisema.
 
"Alifunga magoli mazuri sana. Alionyesha uwezo binafsi kufunga goli la pili. Nafurahi anaonyesha makali yake na hicho ndicho tunahitaji katika safu ya ushambuliaji.
 
"Raheem ana uzoefu na amedhihirisha hilo mara nyingi. Ili kushinda mechi unapokuwa na umiliki wa mpira kwa asilimia 76 sharti ufunge magoli unapopata nafasi. Sterling amedhihirisha kuwa na uwezo huo ila timu yote kwa ujumla wanakosa makali hayo.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Man City - 4
Chelsea - 1
Sare - 0
 

Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 37:

 
Mei 20 Jumamosi
 
2:30pm: Tottenham Hotspur v Brentford
 
5:00pm: Bournemouth v Manchester United
 
5:00pm: Fulham v Crystal Palace
 
5:00pm: Liverpool v Aston Villa
 
5:00pm: Wolverhampton Wanderers v Everton
 
7:30pm: Nottingham Forest v Arsenal
 
Mei 21 Jumapili
 
3:30pm: West Ham United v Leeds United
 
4:00pm: Brighton & Hove Albion v Southampton
 
6:00pm: Manchester City v Chelsea
 
Mei 22 Jumatatu
 
10:00pm: Newcastle United v Leicester City
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 05/19/2023