EPL - Everton v Manchester City


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 36

Everton v Manchester City

Goodison Park
Liverpool, England
Sunday, 14 May 2023
Kick-off is at 15h00 
 
Manchester City watakuwa mgeni wa Everton ugani Goodison Park katika mechi ya ligi mnamo Mei 14 Jumapili ikiwa ni mwendelezo wa juhudi za kutetea taji hilo.
 
The Citizens wanapigiwa upatu kutetea taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kushinda mechi 10 za ligi mfululizo na sasa wanaongoza ligi kwa alama moja.
 
Timu hiyo ya Pep Guardiola ilipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Leeds ugani Etihad Jumamosi iliyopita. Arsenal walishinda mechi yao dhidi ya Newcastle siku iliyofuata ugani St James' Park na kupunguza alama kati yao na City hadi moja.

Dwight McNeil
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
City watachukulia mechi hii kwa uzito mkubwa hasa baada ya the Toffees kuifunga Brighton 5-1 Amnex stadium Jumatatu katika azma yao ya kusalia kwenye ligi kuu na kuepuka shoka la kushuka daraja.
 
Ushindi wa kwanza katika mechi nane za ligi uliinua Everton kutoka nafasi za tatu za mwisho kwenye jedwali na kushika nafasi ya 17, alama mbili juu ya Leicester na Leeds wanaoshika nafasi ya 18 na 19 mtawalia kuelekea mechi tatu za mwisho za msimu.
 
Bournemouth, West Ham, na Nottingham Forest wanashika nafasi za 14, 15 na 16 wakiwa na alama 39, 37 na 33 mtawalia hivyo basi wanasalia katika hatari ya kushuka daraja ukizingatia takwimu.
 
Nyota ya mchezaji Dwight McNeil inazidi kung’aa chini ya Dyche ambaye alikuwa mwalimu wake kwa miaka minne akiwa na klabu ya Burnley. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa na mchango mkubwa majuma ya hivi karibuni huku akifunga magoli 5 katika mechi 9. Alifunga magoli mawili dhidi ya Brighton na kusaidia kupatikana goli moja.

Ilkay Gundogan
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Nahodha wa City Ilkay Gundogan alifunga magoli mawili dhidi ya Leeds wikendi iliyopita. Mchezaji huyo raia wa Ujerumani ameanza mechi 25 katika ligi msimu huu na kupumzishwa mechi 5 tu huku timu hiyo ikizidi kutafuta ubingwa kwenye mashindano matatu; kombe la FA, UEFA na ligi kuu England.
 
Katika vikosi, Everton inawakosa wachezaji kadhaa akiwemo Seamus Coleman, Andros Townsend, Ruben Vinagre, Dele Alli na Ben Godfrey. City itakosa huduma za wachezaji Cole Palmer na Nathan Ake.
 
Dyche alisifia wachezaji wake kwa kuwadhibiti Brighton tangu dakika ya kwanza huku wakifunga magoli matano katika mchezo wa ligi kwa mara ya kwanza tangu Desemba 26 2018 ugenini.
 
"Lilikuwa jambo la kutia moyo kwa sababu tulianza kushambulia moja kwa moja. Tulisambaratisha mbinu na mtiririko wao mapema,” Dyche aliambia evertontv.
 
"Mchezo wa leo ulikuwa tofauti sana. Tumekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kama hizi kwenye michezo iliyopita.
 
"Mechi yetu dhidi ya Leicester ilionyesha ishara ni wapi tunataka kuelekea. Nilizungumza na wachezaj na kuwaambia kuwa tunahitaji kuendeleza juhudi hizi na kuzingatia mbinu katika mechi zijazo. Nilifurahishwa sana na uchezaji wetu.”  
 
Guardiola alimsifia mchezaji Gundogan alipoonyesha mchezo mzuri kama kiungo mkabaji badala ya Rodrigo huku Pep akimtaja mjerumani huyo miongoni mwa wachezaji wazuri aliofundisha.
 
"Gundogan alicheza katika nafasi hiyo msimu tuliposhinda taji la pili la ligi kwani Fernandinho alikuwa majeruhi kwa muda mrefu. Alicheza kwa ueledi mkubwa,” alisema Guardiola.
 
"Nilihisi bila yeye hatungeshinda ubingwa huo. Ni mchezaji mzuri mwenye maarifa na ushindani. Anafanya maamuzi mazuri hata chini ya shinikizo.
 
"Ni mmoja kati ya wachezaji wazuri niliofundisha katika maisha yangu kama kocha. Anaelewa mchezo vizuri.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Everton - 0
Man City - 4
Sare - 1
 

Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 36:

 
Mei 13 Jumamosi
 
2:30pm: Leeds United v Newcastle United
 
5:00pm: Aston Villa v Tottenham Hotspur
 
5:00pm: Chelsea v Nottingham Forest
 
5:00pm: Crystal Palace v Bournemouth
 
5:00pm: Manchester United v Wolverhampton Wanderers
 
5:00pm: Southampton v Fulham
 
Mei 14 Jumapili
 
4:00pm: Brentford v West Ham United
 
4:00pm: Everton v Manchester City
 
6:30pm: Arsenal v Brighton & Hove Albion
 
Mei 15 Jumatatu
 
10:00pm: Leicester City v Liverpool
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 
 

Published: 05/12/2023