CAF Confederation - Yanga SC v Marumo Gallants


BAADA ya kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kocha Mkuu wa Yanga SC Nasreddine Nabi, amesema kuwa sasa ameanza kuwapigia hesabu wapinzani wao Marumo Gallants.
 
Marumo Gallants  wametinga hatua ya nusu fainali baada ya kuiondoa Pyramids FC  kwa mabao 2-1 wakianza na sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa 30 June nchini Misri na baadae kushinda 1-0 nchini Afrika Kusini.
 
Yanga SC juzi wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ikiwa ni timu ya pili kwenye historia za CAF kutoka  Tanzania kutinga hatua hiyo baada ya kuibuka na jumla ya ushindi wa mabao 2-0 na Rivers United.
 
Timu ya kwanza ilikuwa Simba SC walipofanya hivyo mwaka 1974 walipofuzu hatua ya nusu fainal kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya kuja kuingia Fainal ya Kombe la CAF mwaka 1993.
 
Nabi alisema mechi yao ilikuwa ya ushindani mkubwa alitambua wapinzani wake hao wangekuja kucheza na ikamlazimu kucheza kwa kukaba zaidi.
 
“ Mechi ilikuwa ngumu tangu awali nilisema kuwa Rivers hawana cha kupoteza wangecheza mpira, ikatulazimu kucheza kwa kuzuia kwa sababu ningefuka wangepata bao la kwanza na baadae wangefunga la pili.
 
Hatukucheza kwa kukaba pekee bali niliweka washambuliaji ili tukipata nafasi tuweze kufunga na tulitengeneza nafasi mbili hatukuweza kuzitumia.
 
Mechi iliyopita tulitengeneza nafasi mbili ugenini na kufanikiwa kushinda, mechi hii tulitengeneza nafasi tano lakini hatukuzitumia, tungefunguka basi tungepoteza mchezo. Hizi mechi nimewahi kushuhudia kushinda ugenini na kufungwa nyumbani,” alisema kocha huyo
 
Nabi alisema kuhusu mikakati yangu ya hatua ya nusu fainali inaendelea kwani kwa sasa hana muda wa kupumzika kwa kuwa anauhakika wa kuendelea mbele mpaka Fainali.
 
"Sijajua hadi sasa (juzi) nakutana na nani kati ya Marumo Gallants au Pyramids, itanilazimu kabla ya kuanza mipango ya mechi hiyo lazima niwafatilia wapinzani wangu ubora na madhaifu yao,” alisema Kocha huyo.
 
Aliongeza haitoshi kuangalia hayo pia mbinu za kiufundi wanavyocheza ugenini na nyumbani wanakuwaje ili kuanza rasmi mipango yao kuelekea mchezo huo wa nusu fainali
 
“Kazi nitaanza kuifanya baada ya mchezo huu na kuona wapinzani wetu hao na kuanza kujua ni jinsi gani ya kujipanga na kuingia kwa mfumo gani katika mchezo wetu huo tutakaoanzia nyumbani,” alisema Nabi.
 
Alisisitizia kuwa kila mechi wanaingia na mipango yake, mikakati aliyoingia nayo katika robo fainali itakuwa tofauti na atakavyocheza nusu fainali.
 
 
Yanga SC itaikaribisha Marumo Gallants inayonolewa na kocha wa zamani wa Simba SC Dylan Kerr, mechi itakayochezwa Jumatano tarehe 10 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
 
Kuelekea mechi hiyo, Tayari Shirikisho la Soka nchini (TFF), limetangaza kuusogeza mbele mchezo wa Kombe la Shirikisho ASFC kati ya Yanga SC dhidi ya Singida Big Stars.
 
Taarifa kutoka ndani ya Shirikisho hilo, inasema kuwa wamefanya hivyo kuipa muda mzuri Yanga SC kujiandaa na mechi hiyo muhimu kwao na nchi kwa ujumla.
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 05/05/2023