Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 PGA Championship
US PGA Tour
Southern Hills Country Club
Tulsa, Oklahoma, USA
19 - 22 May 2022
Tiger Woods anatarajia kushinda shindano la gofu la
2022 PGA na kufuata nyayo za wakongwe wa mchezo huo Walter Hagen na Jack Nicklaus.
Nyota huyo wa gofu kutoka Marekani ameshinda shindano hilo mara nne; 1999, 2000, 2006 na 2007. Ni wachezaji wawili tu walioshinda shindano hili zaidi yake
Mmarekani mkongwe Hagen ameshinda shindano hilo mara tano kama alivyofanya raia mwenzake Nicklaus ingawaje mafanikio yao yalikuja katika nyakati tofauti.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
Woods alirejea kwenye gofu katika shindano la Masters mwezi Machi mwaka huu baada ya kupata ajali mbaya ya gari na kupata majeraha ya miguuni kule California Februari 2021.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 46 aliwashinda wachezaji mahiri kama Jordan Spieth, Brooks Koepka, Xander Schauffele na Bryson DeChambeau katika shindano hilo la Masters.
Woods alipata alipata alama 78-78 ambazo ni alama za juu kwake katika shindano la Master. Hata hivyo, ushindi mkubwa ulikuwa yeye kurejea kwenye mchezo huo baada ya kupata ajali mbaya.
Woods ambaye ni mchezaji wa mwaka wa PGA Tour kwa mara 11 anatarajia kushinda shindano la 16 kubwa kwa kuibuka na ushindi wa PGA championship na kuikaribia rekodi ta Nicklaus ya mataji 18.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Tulianza mazoezi kama wiki moja hivi iliyopita. Nilicheza gofu kidogo na nilijihisi vizuri,” alisema Woods.
“Naamini nitaendelea kuimarika zaidi kiafya kadri ninavyofanya mazoezi japokuwa sidhani nitakuja kuwa asilimia mia moja.
"Nitazidi kuimarika. Nafurahia wiki hii. Japokuwa sitacheza sana, kila wakati nikipata nafasi ya kucheza na kushindana nitafurahi,” aliongeza.
"Ni mechi kubwa kama hizo tu unazoweza kucheza nyumbani.”
Washindi watano wa mwisho wa PGA Championship
2017 - Justin Thomas - Marekani
2018 - Brooks Koepka - Marekani
2019 - Brooks Koepka - Marekani
2020 - Collin Morikawa - Marekani
2021 - Phil Mickelson - Marekani
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.