Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 FIA Formula One World Championship
2022 Miami Grand Prix
Miami International Autodrome
Miami Gardens, Florida, United States
Sunday, 8 May 2022
Dereva wa Red Bull Racing Max Verstappen atatazamia kumshinikiza zaidi Charles Leclerc wa Ferrari kwenye mbio za
Miami Grand Prix mnamo Jumapili Mei 8.
Bingwa huyo mtetezi wa mbio za Formula One duniani alianza msimu huu kwa kusuasua alipomaliza kwenye nafasi ya 19 katika mbio za kwanza za msimu ambazo ni Bahrain Grand Prix.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Verstappen alijirudi na kupata ushindi wa Saudi Arabia Grand Prix pamoja na Emilia Romagna Grand Prix, kabla ya kulazimika kukatisha mbio za Australian Grand Prix kutokana na hitilafu ya mitambo ya mafuta zilizosababisha moto kwenye gari kwenye mzunguko wa 39.
Raia huyo wa Uholanzi anashikilia nafasi ya pili kwenye jedwali la madereva akiwa na alama 59, alama 27 nyuma ya kiongozi Leclerc baada ya mbio nne. Verstappen alipunguza nafasi baina yake na kiongozi wa sasa aliyemaliza katika nafasi ya sita Imola kutokana na makosa ya uendeshaji.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Verstappen ana imani kuwa Red Bull wamerekebisha hitilafu za mafuta lakini anakiri kuwa kuna uwezekano wa hitilafu nyingine kutokea kwenye mkondo wa Miami ukizingatia itakuwa ni mbio za kwanza za Formula One katika mkondo huo.
"Hitilafu hutokea wakati wowote lakini timu hii imeonyesha uwezo wa kutatua matatizo,” alisema dereva huyo mwenye umri wa miaka 24. “Tunahitaji umakini huo. Tayari nimelazimika kustaafu mara mbili kwenye mbio za kwanza nne na sio jambo zuri iwapo tunahitaji ubingwa.
"Tulifanya vizuri sana kwenye mbio za Italia. Gari lilikuwa dhabiti na hatukufanya makosa. Ilikuwa muhimu sana lakini mkondo wa Miami unaibua maswali kwa watu wengi.
"Unaweza ukafanya vizuri sana kwenye mkondo mmoja kisha ukafeli sana kwenye mkondo tofauti wiki moja baadaye. Hili linachangiwa na mambo madogo kwa mfano magurudumu kukosa kushika barabara vizuri. Ferrari walikuwa wa kwanza Imola. Mimi na Charles Leclerc tulikuwa pamoja kwenye mbio za Jumamosi lakini magurudumu yake yakagoma.
"Hicho ndicho kilichotutokea Melbourne na ndio sababu ya mkondo wa Miami kutiliwa shaka na watu wengi.”
Matokeo ya 2022 ya mbio za Emilia Romagna Grand Prix
Mshindi: Max Verstappen - Red Bull Racing
Nafasi ya pili: Sergio Perez - Red Bull Racing
Nafasi ya tatu: Lando Norris - McLaren-Mercedes
Bashiri Motosport na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni soka, motorsport, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.