Verstappen apania taji la pili Spanish Grand Prix


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 FIA Formula One World Championship 

Six Round

2022 Spanish Grand Prix

Circuit de Barcelona-Catalunya
Montmeló, Spain
Sunday, 22 May 2022
 
Max Verstappen atafanya kila awezalo kushinda kwa mara ya pili mbio za langa langa za Spanish Grand Prix mnamo Mei 22.
 
Dereva huyo wa Red Bull Racing-RBPT alikosa taji la mbio hizo mwaka jana kwa nafasi ndogo sana alipomaliza katika nafasi ya pili lakini alifanikiwa kushinda taji hilo mwaka 2016.
 
Verstappen yupo katika hali nzuri sana mwaka huu, huku akishinda mbio za hivi maajuzi za msimu huu ambazo ni Miami Grand Prix 2022 Mei 8.

Sergio Perez
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Verstappen ambaye ni bingwa mtetezi wa mashindano ya Formula One alifanya juhudi nyingi kumpita dereva wa Ferrari Charles Leclerc mwanzoni mwa mbio na kukaa katika nafasi hiyo ya kwanza hadi kushinda mbio hizo.
 
Madereva wa Ferrari Leclerc na Carlos Sainz Jr walimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia kwenye mbio za Marekani, yakiwa ni mafanikio makubwa kwa kampuni hiyo ya Italia.
 
Hata hivyo, Leclerc anashikilia nafasi ya kwanza kwenye jedwali la madereva la 2022 huku Verstappen akiwa katika nafasi ya pili ikiwa ni mbio tano baada ya kuanza kwa msimu huu.
 
Verstappen ambaye alishinda mbio za Emilia Romagna Grand Prix kabla ya kuibuka na ushindi kwenye mbio za Miami Grand Prix, ana uhakika wa kushinda mbio za Uhispania na kupunguza nafasi iliyopo kati yake na Leclerc.

Carlos Sainz
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
“Ndio, zilikuwa mbio nzuri. Sikufanya mbio za majaribio. Sikufahamu nini cha kutarajia kwenye mbio zenyewe,” alisema Verstappen baada ya kushinda mbio za Miami Grand Prix.
 
"Tulikuwa na mwanzo mzuri. Niliona nafasi ya kupenya kwa nje dhidi ya Sainz kwenye mzunguko wa kwanza. Nilijaribu na nikafanikiwa. Sikufurahishwa na gari la usalama hata hivyo.
 
"nilielewa kilichofanyika. Siwezi kulalamika sana kwa sababu nimefaidika kwa njia moja au nyingine kwenye mbio za nyumba,” aliongeza.
 
"Nilifahamu fika kuwa haitakuwa rahisi toka mwanzo hadi mwisho. Ilihitaji nguvu nyingi. Mizunguko kumi ya mwisho haikuwa rahisi hata kidogo ukizingatia sakafu ilivyo.”
 
Ferrari inaongoza kwenye jedwali na waundaji, wakifuatiwa na Red Bull Racing-RBPT huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Mercedes.
 

Matokeo ya mbio za Spanish Grand Prix 2022

 
Mshindi: Lewis Hamilton - Mercedes 
Nafasi ya pili: Max Verstappen of Red Bull Racing-Honda 
Nafasi ya tatu: Valtteri Bottas - Mercedes 
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 
 
 

Published: 05/20/2022