Ushindi wa City dhidi ya Aston Villa kuwapa ubingwa


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English Premier League

Matchday 38

Manchester City v Aston Villa

Etihad Stadium
Manchester, England
Sunday, 22 May 2022
Kick-off is at 18h00  
 
Manchester City watatarajia kushinda taji la ligi kwa mara ya sita ndani ya miaka 11 watakapoialika Aston Villa ugani Etihad Mei 22 Jumapili ambayo itakuwa ni siku ya mwisho ya msimu.
 
The Citizens wana uwezo wa kuamua hatma yao ya kushinda ligi kwani ushindi dhidi ya Villa utawapa ubingwa bila kuzingatia matokeo ya Liverpool na Wolves.
 
Vijana wa Pep Guardiola walikosa nafasi ya kuongeza alama zaidi baada ya kutoa sare ya 2-2 dhidi ya West Ham Jumapili iliyopita.

Pep Guardiola
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Guardiola anasubiri nafasi ya kusherehekea ushindi wa taji mbele ya mashabiki wa nyumbani na kuongeza kuwa wachezaji wake watafanya kila wawezalo kupata mafanikio hayo.
 
"Tunachotakiwa ni kushinda mechi yetu la sivyo Liverpool watakuwa mabingwa,” alisema raia huyo wa Uhispania. “Nawahakikishia ndani ya wiki moja tiketi zitakuwa zimeuzwa nyingi sana. Tutapambana sote kupata mafanikio haya.
 
"Ushindi huu utakuwa mafanikio makubwa baada ya miaka mingi tukiwa pamoja. Itapendeza sana kushinda mechi moja na kusherehekea na mashabiki wetu kwa kuwa mabingwa.”
 
Aston Villa wapo katika nafasi ya 13 katika jedwali la ligi baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Crystal Palace wikendi iliyopita japokuwa wana uwezo wa kumaliza katika nafasi ya tisa.

Steven Gerrard
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Vijana wa Steven Gerrard walikaribia kushinda mechi ya tatu mfululizo katika mechi nne Ollie Watkins alipofunga bao la dakika 69 kabla ya Jeff Schlupp kusawazisha dakika tisa kabla ya mchezo kuisha.
 
"Tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini tulifanikiwa kushinda goli moja tu leo,” alisema Gerrad.
 
"Tulicheza kama tulivyopanga lakini hatukupata matokeo. Tulifanya makosa na tulishindwa kuzuia vizuri. Tutajilaumu wenyewe kuliko wapinzani wetu.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi

Mechi - 5
Man City - 5
Aston Villa - 0
Sare - 0


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 05/17/2022