Torino kupambana na Napoli


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Italian Serie A

Matchday 35

Torino FC v SSC Napoli 

Stadio Olimpico Grande Torino 
Torino, Italy 
Saturday, 7 May 2022
Kick-off is at 21h45  
 
Torino FC watakuwa mwenyeji wa SSC Napoli kwenye mechi ya ligi kuu ya Italia ugani Stadio Olimpico Grande Torino Mei 7.
 
Torino walipata ushindi wa 3-1 ugenini dhidi ya Empoli FC kwenye mechi ya ligi iliyochezwa Mei 1.
 
Torino wameshinda mechi tatu za ligi na kupata sare tatu katika mechi sita zilizopita za ligi.

Simone Zaza
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Vile vile, the Maroons hawajashindwa katika mechi tatu za ligi walizocheza nyumbani huku wakishinda mechi moja na kupata sare mbili mfululizo.
 
Kwingineko, Napoli walipata ushindi mkubwa wa 6-1 dhidi ya US Sassuolo katika mechi ya ligi iliyopita ya Aprili 30.
 
Kabla ya mechi hiyo, Napoli walikuwa hawajapata ushindi kwenye mechi tatu za awali huku wakipata sare moja na kushindwa mechi mbili.
 
Kwenye mechi ya mwisho ya ligi ugenini, Napoli walishindwa na Empoli ambao walikatisha msururu wa mechi tisa ugenini bila kushindwa kwa upande wa Napoli.


Jonathan Ikone
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Kuwa na uhakika wa kucheza ligi ya mabingwa zikiwa zimebaki mechi tatu haikuwa rahisi,” alisema meneja wa Napoli Luciano Spalletti baada ya kuishinda Sassuolo.
 
"Hata hivyo kuna majuto. Nilizungumzia kuhusu taji la ligi ili kuwapa motisha lakini kupata ushindi wa mechi kwenye mazingira ya leo ambapo baadhi ya mashabiki wananung’unika ni jambo linaloniuma kwa sababu wachezaji hawa wamepigania timu hii kwa nguvu nyingi msimu huu.”
 
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya Torino na Napoli ilikuwa Oktoba 17 2021.
 
Napoli walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Torino kwenye mechi iliyochezwa ugani Stadio Diego Armando Maradona, zamani ukiitwa Stadio Sao Paolo.
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi

Mechi - 5
Torino - 0
Napoli - 3
Sare - 2


Ratiba ya Serie A mchezo wa 36

 
Mei 6 Ijumaa 
 
7:45pm- Inter Milan v Empoli FC 
 
10:00pm- Genoa CFC v Juventus 

 
Mei 7 Jumamosi
 
4:00pm- Torino FC v SSC Napoli
 
7:00pm- US Sassuolo v Udinese Calcio 
 
9:45pm- SS Lazio v UC Sampdoria 

 
Mei 8 Jumapili
 
13:30pm- Spezia FC v Atalanta BC 
 
4:00pm- Venezia FC v Bologna FC 
 
7:00pm- US Salernitana  v Cagliari Calcio 
 
9:45pm- Hellas Verona v AC Milan 

 
Mei 9 Jumatatu 
 
9:45pm- ACF Fiorentina v AS Roma


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 05/06/2022