Thomas atazamia ushindi mwingine, shindano la gofu la Charles Schwab Challenge


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 Charles Schwab Challenge 

US PGA Tour 

Colonial Country Club
Fort Worth, Texas, USA  
26 - 29 May 2022 
 
Justin Thomas anatarajia kuendeleza msururu wa matokeo mazuri kwenye shindano la gofu la Charles Schwab Challenge baada ya kushinda shindano la hivi maajuzi katika ratiba ya 2021-22 PGA Tour.
 
Raia huyo wa Marekani alishinda shindano la pili kubwa na shindano la pili la PGA kwa kumshinda Will Zalatoris kwenye mchujo Southern Hills Country Club mnamo Mei 22.
 
Thomas ameshinda mashindano 15 kwenye msururu wa PGA Tour na kuweka historia aliposhinda shindano la 104 la PGA.
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alitoka nyuma mwanzoni mwa hawamu ya mwisho na kushinda. Anashikilia kwa pamoja rekodi ya mchezaji aliyetoka nyuma na kushinda katika historia ya shindano hili.
 
Thomas anashikilia nafasi ya tano kwenye jedwali rasmi la gofu duniani na pia ni mchezaji namba moja wa dunia wa zamani baada ya kushinda msururu wa PGA wa 2017.
 
Kabla ya kushinda wikendi iliyopita, Thomas alikuwa amemaliza katika nafasi ya tano kwenye shindano la 2022 AT&T Byron Nelson ambapo K.H Lee alitetea taji lake kwa mafanikio mnamo Mei 15.
 
Mchezaji huyo aliyeshinda hela nyingi kwenye PGA Tour ya 2017 na 2018 alimaliza katika nafasi ya 40 kwenye shindano la gofu la Charles Schwab Challenge mwaka jana atakuwa na hamu ya kushinda shindano hilo kwa mara ya kwanza wikendi hii.

K.H Lee
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Sikuangalia kibao cha matokeo leo. Nilipata ishara kutokana na kushangilia kwa mashabiki kuwa nilikuwa nafanya vizuri,” alisema Thomas baada ya kushinda shindano la gofu la PGA mwaka 2022.
 
"Nafahamu kuwa wachezaji wote waliokuwa mbele yangu ni wachezaji mahiri lakini hawajashinda shindano kubwa. Ulikuwa wakati muhimu.
 
"Nilikuwa nimeshtuka, nahisi hata wao walikuwa wameshituka vile vile. Nilijiambia kwamba nitafanya kilicho ndani ya uwezo wangu; kama kitafaa nitashukuru, kama hakitatosha kunipa ushindi basi kuna nafasi nyingine.”
 
Ben Hogan ni mchezaji mwenye historia kubwa ya ushindi katika shindano hili la Charles Schwab Challenge ikiwa ameshinda mara tano.
 

Washindi watano wa mwisho wa Charles Schwab Challenge

 
2016 - Kevin Kisner - Marekani 
2018 - Justin Rose - Uingereza
2019 - Kevin Na - Marekani  
2020 - Daniel Berger - Marekani  
2021 - Jason Kokrak - Marekani 
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 
 
 

Published: 05/26/2022