Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Italian Serie A
Matchday 38
US Sassuolo v AC Milan
MAPEI Stadium
Reggio nell'Emilia, Italy
Sunday, 22 May 2022
Kick-off is at 19h00
US Sassuolo watamwalika AC Milan kwenye mechi ya ligi ya
Serie A ugani MAPEI Stadium mnamo Mei 22.
Sassuolo wakiwa ugenini walipata ushindi muhimu wa 3-1 dhidi ya Bologna katika mechi ya ligi iliyopita ya Mei 15.
Sassuolo hawajashindwa katika mechi mbili za ligi zilizopita baada ya kuandikisha ushindi wa mechi moja na sare moja.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Hata hivyo, Sassuolo hawajashinda mechi yoyote ya ligi kati kati ya mechi mbili za mwisho ugenini huku wakishindwa mechi moja na kupata sare moja.
Kwingineko, AC Milan walishinda mechi yao ya ligi 2-0 nyumbani dhidi ya Atalanta BC. Mechi hiyo ilichezwa Mei 15.
Milan hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika mechi 15 za ligi zilizopita huku wakiandikisha sare tano na kupata ushindi katika mechi 10.
Vile vile, Milan hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika mechi 11 zilizopita wakiwa ugenini huku wakipata sare tatu na ushindi mara nane.
Ushindi wa aina yoyote utaipa Milan taji la ligi.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Ni lazima tujiandae wiki hii kama tunavyojiandaa katika wiki zilizopita,” alisema meneja wa Milan Stefano Pioli.
“Nilipoulizwa kwenye mkutano na wanahabari lengo letu lilikuwa lipi, ilikuwa wazi kabisa kwetu kwamba tuzidi alama 79 tulizopata mwaka uliopita.
"Tulifahamu wazi kwa kuimarisha matokeo yetu tunaweza kupata mafanikio mengine. Tutajituma zaidi. Hatuna nafasi ya kuzembea na kufikiria kwamba ligi imekamilika kwa sababu Sassuolo ina wachezaji wenye uwezo mkubwa.”
Mchezo wa mwisho wa ligi baina ya Sassuolo na Milan ulikuwa Novemba 28 2021.
Sassuolo walipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Milan kwenye mechi hiyo iliyochezewa ugani Stadio Giuseppe Meazza ambao umekuwa mwenyeji wa fainali za UEFA mara nne.
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi
Mechi - 5
Sassuolo - 2
Milan - 2
Sare - 1
Ratiba ya Serie A mchezo wa 38.
Mei 20 Ijumaa
9:45pm- Torino FC v AS Roma
Mei 21 Jumamosi
6:45pm- Genoa CFC v Bologna FC
9:45pm- Atalanta BC v Empoli FC
9:45pm- ACF Fiorentina v Juventus FC
9:45pm- SS Lazio v Hellas Verona
Mei 22 Jumapili
01:00pm- Spezia FC v SSC Napoli
7:00pm- US Sassuolo v AC Milan
7:00pm - Inter Milan v UC Sampdoria
7:00pm- Venezia FC v Cagliari Calcio
7:00pm - US Salernitana v Udinese Calcio
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.