Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 AT&T Byron Nelson
US PGA Tour
TPC Craig Ranch
McKinney, Dallas, Texas, USA
12 - 15 May 2022
Scottie Scheffler anapigiwa upatu kushinda taji la gofu la AT&A Byron Nelson mwaka 2022 litakaloandaliwa TPC Craig Ranch.
Raia huyo wa Marekani yupo katika msururu wa matokeo mazuri kwa sasa ikiwa ameshinda mashindano manne ya PGA Tour ya mwaka 2022 na anashikilia nafasi ya kwanza katika jedwali rasmi la shirikisho la gofu duniani.
Scheffler ni mshindi wa taji la gofu la Waste Management Phoenix Open, Arnold Palmer Invitational, WGC-Dell Technologies Match na vile vile shindano la Masters.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Ushindi wa mwisho wa mwanafunzi huyo wa zamani wa chuo kikuu cha Texas ulikuwa mwezi jana kwenye shindano la Masters alipomshinda Rory McIlroy kwa matundu matatu.
Scheffler amekuwa mchezaji wa gofu wa wa tano kucheza shindano la Masters akishikilia nafasi ya kwanza kwenye jedwali la dunia la gofu na kuibuka na ushindi.
Scheffler ambaye ni mzaliwa wa New Jersey anaungana na Ian Woosnam (1991), Fred Couples (1992), Tiger Woods (2001, 2002) na Dustin Johnson (2020) kwenye orodha hiyo.
Scheffler pia amekuwa mchezaji gofu wa kwanza tangu Arnold Palmer mwaka 1960 na wa pili katika historia kushinda mashindano manne ikiwemo Masters kwa muda huo baada ya kuanza kwa msimu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Nadhani kwa sababu ni Masters. Nilikuwa na ndoto ya kushiriki shindano hili,” alisema Scheffler baada ya kushinda Masters.
"Nilihisi machozi nilipopata mwaliko wangu wa kwanza kwa njia ya barua pepe. Napenda shindano hili. Huwezi kujua utapata nafasi ngapi.
"Hujui utapata nafasi bora kuliko hii. Unapaswa kuzitumia ipasavyo.”
Tom Watson ni mchezaji aliye na mafanikio mengi zaidi katika historia ya AT&A Byron Nelson akiwa ameshinda shindano hili mara nne.
Washindi 5 wa mwisho wa AT&A Byron Nelson
2016 - Sergio Garcia - Uhispania
2017 - Billy Horschel - Marekani
2018 - Aaron Wise - Marekani
2019 - Sung Kang - Korea Kusini
2021 - K.H Lee - Korea Kusini
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.