Reds na Whites kupigania ufalme wa Ulaya


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 UEFA Champions League

Final

Liverpool v Real Madrid

Stade de France
Paris, France
Saturday, 28 May 2022
Kick-off is at 22h00  
 
Liverpool na Real Madrid watakutana kwenye fainali ya ligi ya UEFA kwa mara ya tatu ugani Stade de France mnamo Mei 28 Jumamosi.
 
Miamba hao wawili wa soka la Ulaya walikutana mara ya mwisho kwenye fainali hii miaka minne iliyopita ambapo Real Madrid walipata ushindi wa 3-1 mjini Kyiv na kunyanyua taji hilo kwa mara ya 13.
 
The Reds walipata ushindi wa 1-0 timu hizo zilipokutana kwenye fainali ya kwanza kabisa baina yao mwaka 1981 ugani Parc des Princes mjini Paris na kunyanyua taji hilo mara ya tatu.

Luka Modric
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Hii itakuwa mara ya 17 kwa Real Madrid kufika fainali ya shindano hili, ambayo ni mara nyingi zaidi kuliko timu yoyote.
 
The Reds wanapania kunyanyua taji hili kwa mara ya saba, ambapo wataungana na AC Milan na kuchukua nafisi ya pili kwenye orodha ya mabingwa wa zamani.
 
Vijana wa Klopp waliongoza kundi B lililojumuisha Atletico Madrid, FC Porto na Milan kwa kushinda mechi zote sita. Waliwaondoa Inter Milan kwenye hatua ya 16 kwa mabao 2-1 kabla ya kuwabwaga Benfica (6-4) ndani ya mechi mbili na Villarreal (5-2) kwenye mechi mbili, katika robo fainali na nusu fainali mtawalia.
 
Kwa urahisi, timu ya Carlo Ancelotti ilishinda kundi D ambalo lilikuwa na Inter, Sheriff Tiraspol na Shakhtar Donetsk. Kwenye hatua ya 16, Madrid iliwaondoa PSG kwa jumla ya 3-2 na vile vile kuwaondoa Chelsea kwa jumla ya 5-4 na Manchester City kwa jumla ya 6-5 kwenye robo na nusu fainali mtawalia.

Jordan Henderson
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson amewaasa wachezaji wenzake kusahau machungu ya kupoteza taji la ligi ya premier kwa Man City na badala yake kuwekeza nguvu zote kwenye mechi ya fainali itakayochezewa mji mkuu wa Ufaransa.
 
"Tuangazie changamoto iliyopo mbele yetu wiki ijayo. Ni mechi kubwa dhidi ya mpinzani mkubwa. Ni sharti tuwe katika ubora wetu iwapo tunataka kuwa mabingwa.
 
"Najivunia sana wachezaji hawa lakini kuna kazi kubwa mbele yetu. Tuna mechi dhidi ya Real Madrid wiki ijayo.”
 

Takwimu baina ya timu hizi mbili

Mechi - 7
Liverpool - 2
Real Madrid - 4
Sare - 1

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 05/26/2022