Reds na Spurs kung’ang’ania alama muhimu


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English Premier League

Matchday 36

Liverpool v Tottenham Hotspur

Anfield
Liverpool, England
Saturday, 7 May 2022
Kick-off is at 21h45  
 
Liverpool wanapania kuwashinikiza Manchester City watakapoalika Tottenham ugani Anfiled kwenye mechi ya ligi mnamo Mei 7.
 
The Reds walipata uongozi wa ligi japo kwa muda mfupi tu walipoishinda Newcastle 1-0 ugani St James' Park Jumamosi iliyopita kabla ya City kupata ushindi wa 4-0 dhidi ya Leeds na kurudi kileleni.
 
Vijana wa Jurgen Klopp wapo nyuma ya City kwa alama moja tu huku zikiwa zimesalia mechi nne tu msimu kukamilika. Zaidi ya mechi za ligi, kuna mechi za EFL na mechi za UEFA pia.
 
Timu hiyo ya Merseyside itacheza fainali ya kombe la FA dhidi ya Chelsea na wanaongoza kwa mabao mawili dhidi ya villlareal kabla ya mechi ya marudiano ya nusu fainali ya ligi ya UEFA.

Jurgen Klopp
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Klopp amekiri kuwa kuna furaha kubwa kwa wanaliverpool muda huu lakini makossa madogo yanaweza kusababisha madhara makubwa.
 
"Tuna furaha kubwa. Napenda timu hii na tunacheza kila mechi vizuri iwezekanavyo na huo ndio mpango wetu,” alisema mjerumani huyo.
 
"Tuko katika hali nzuri lakini bado tunazo mechi nyingi za kucheza bila kujali mechi za UEFA. Tutajaribu kushinda mechi zote zilizosalia iwapo tunahitaji ubingwa.”
 
Spurs na Arsenal wanapambania kuingia nafasi ya nne itakayowawezesha kushiriki mechi ya UEFA msimu ujao huku wakiachana kwa alama mbili tu.
 
Vijana wa Antonio Conte walikaa katika nafasi ya nne kwa muda mfupi waliposhinda Leicester 3-1 Jumapili lakini Arsenal ikawaondoa kwa kuishinda West Ham United 2-1.  

Antonio Conte
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Conte amekiri kuwa mechi zote zilizobaki zitakuwa kama fainali kwa sababu wakiteleza kidogo nafasi ya kuingia nne bora itakuwa finyu sana.
 
"Ushindi huu ulikuwa muhimu kwa sababu unatupa nafasi nyingine ya kupigania nafasi ya nne,” alisema raia huyo wa Italia. “Tunatakiwa kupambana hivyo hivyo. Kila mchezaji ni jukumu lake kujituma kwa asilimia 150. Asilimia 100 haitoshi kwa wakati huu.
 
"Zimesalia mechi nne. Inayofuata ni dhidi ya Liverpool. Tutajiandaa vilivyo kwa ajili ya mechi hii na kujaribu kupata alama zote. Kila mechi ni muhimu. Wengi wanafikiri tunafaa kupata alama kwenye mechi nyingine.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi

Mechi - 5
Liverpool - 4
Tottenham - 0
Sare - 1

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 05/06/2022