Quartararo apania ushindi kwa mpigo Italia


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 MotoGP World Championship

2022 Italian Grand Prix

Mugello Circuit
Florence, Italy
Sunday, 29 May 2022
 
Mwendeshaji pikipiki wa Monster Energy Yamaha, Fabio Quartararo anatazamia kushinda mbio za pikipiki za Italian Grand Prix kwa mwaka wa pili mfululizo Jumapili ya Mei 29.
 
Raia huyo wa Ufaransa alipata ushindi wa tatu wa msimu wa 2021 kwenye mkondo wa Mugello huku akivisha taji la dunia kwa mara ya kwanza.


Aleix Espargaro of Aprilia Racing
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Quartararo anaongoza jedwali la waendeshaji kwa alama nne mbele ya Aleix Espargaro wa Aprilia Racing (98) baada ya hawamu sita na amemaliza kwenye jukwaa mara tatu.
 
Matokeo mazuri yaliyoandikishwa na mwendeshaji huyo mwenye umri wa miaka 23 yalikuwa ni ushindi kwenye mbio za Portuguese Grand Prix na kupata P4 kwenye mbio za French Grand Prix.


Enea Bastianini
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Quartararo alikiri kuwa hakuweza kuwapita waendeshaji wengine kule Le Mans kwa sababu alitumia muda mwingi nyuma ya Espargaro.
 
"Sijafurahishwa na uendeshaji wangu hata kidogo. Kulikuwa na ajali tatu mbele yangu. Nafasi yangu haikufaa kuwa ya nne, pengine nyuma zaidi,” alisema.
 
"Haikuwa kasi yetu hiyo. Kwenye mbio za majaribio, ukiangalia tulikuwa na kasi nzuri. Kwenye mbio zenyewe, unapokuwa kwenye nafasi ambayo huwezi kumpita aliye mbele yako, nafasi ya ushindi inakuwa finyu.
 
"Ndio maana sijalalamika kwa sababu ni vitu ambavyo nimezoea kwa kiasi fulani. Najaribu kujituma asilimia mia kila wakati kama nilivyofanya leo. Kuna wakati nilipoteza kasi kidogo na Aleix akanipita. Baada ya mizunguko mitano nilikuwa nimemfikia tena.
 
"Tulikuwa na kasi kubwa sana na kwenye hali hiyo ni vigumu kumpita mwezako. Kwenye mbio yote hatukuweza kumpita mtu hata mmoja. Nilikofanikiwa ni kutokana na makosa ya mwendeshaji. Kulikuwa na ajali tatu mbele yangu, Marc Marquez alipita upande wa nje kidogo lakini sikupita mtu katika mbio.”
 

Matokeo ya mbio za French Grand Prix 2022

 
Mshindi: Enea Bastianini - Gresini Racing
Nafasi ya pili: Jack Miller - Ducati Lenovo Team
Nafasi ya tatu: Aleix Espargaro - Aprilia Racing
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 05/26/2022