Nadal kuendelea na ubabe wake Roland Garros


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 Roland Garros 

ATP Tour & WTA Tour 

Stade Roland Garros 
Paris, France
22 May - 5 June 2022
 
Rafael Nadal anapania kuendeleza ubabe wake kwenye shindano la tenisi la Roland Garros kwa kushinda shindano la mwaka huu mnamo Juni 5.
 
Kwa sasa, Nadal anashikilia nafasi ya tano kwenye jedwali la dunia la bodi ya usimamizi wa tenisi (ATP) na ndiye mchezaji aliye na mafanikio makubwa kwenye historia ya shindano hili duniani baada ya kushinda mara kumi na tatu.
 
Raia huyo wa Uhispania ameweka rekodi ya kushinda mara 21 kwenye mashindano ya Grand Slam ya mchezaji mmoja kila upande kwa wanaume, huku mara 62 ikitokea kwenye sakafu ya udongo ambapo alipata jina la utani la “The King of Clay.”

Diego Schwartzman
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 

Nadal aliingia kwenye shindano la mwaka 2021 la Roland Garros akipigiwa upatu, akitarajia kuwa mwanamme wa kwanza kushinda shindano hilo mara ishirini na moja.
 
Nadal alifika nusu fainali kwa kumshinda Jannik Sinner na Diego Schwartzman, na kukutana na Novak Djokovic kwenye fainali kama ilivyokuwa mwaka 2020.
 
Mshindi huyo wa dhahabu katika mashindano ya olimpiki, na anayejulikana kwa kasi na uwezo mkubwa uwanjani alishindwa na Djokovic kwa seti nne. Hii ilikuwa ni mara yake ya tatu kushindwa katika historia ya mashindano ya tenisi ya Roland Garros.
 
Hata hivyo, Nadal alishinda shindano lake kubwa la 21 mapema mwaka huu aliposhinda kwa seti tano shindano la tenisi la Australian Open baada ya kuwa chini kwa seti mbili. 


Daniil Medvedev
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alisema kuwa atakuwa anauguza jeraha katika mashindano ya mwaka huu ya Roland Garros na kwamba atakuwa na daktari kwa ukaribu wakati wa mchezo.
 
"Jambo la kwanza ni kuhakikisha kuwa sina uchungu wakati wa mechi ya majaribio. Nitakuwa na daktari wangu kwa ukaribu katika mashindano ya French Open na Roland Garros,” alisema Nadal.
 
"Ni muhimu kwa sababu chochote kinaweza kutokea. Unatakiwa kuzingatia kilichotokea wakati ulikuwa asilimia mia na wakati kulikuwa na tatizo kwa umakini.” 
 
Hela itakayoshindaniwa kwenye shindano la mwaka 2022 la Roland Garros itakuwa Euro milioni 43.6. Washindi wa shindano la mchezaji mmoja kila upande kwa wanaume na wanadada mjini Paris watapokea Euro milioni 2.2 kila mmoja. 
 
Fainali ya 2021, shindano la mchezaji mmoja kila upande Roland Garros, wanaume
Novak Djokovic alimshinda Stefanos Tsitsipas
 
Fainali ya 2021, shindano la mchezaji mmoja kila upande Roland Garros, wanawake
Barbora Krejčíková alimshinda Anastasia Pavlyuchenkova


Bashiri tenisi mtandaoni

Bashiri manguli kwenye michuano bora ya tenisi kutoka Wimbledon hadi Roland Garros. Jisajili leo na anza kubashiri kwenye machaguo tofauti ambayo tenisi inakupatia; kutoka 1x2 matokeo ya mechi, bashiri kwa mchezaji wako unayempenda hadi kwenye bashiri nyingi kama Mshindi wa Set. Chochote unachochagua kufanya, Betway ina chaguo kwaajili yako.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway
 

Published: 05/20/2022