Milan wapania kuisulubu Atalanta.


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Italian Serie A

Matchday 37

AC Milan v Atalanta BC

Stadio Giuseppe Meazza 
Milano, Italy 
Sunday, 15 May 2022
Kick-off is at 19h00  
 
AC Milan watakuwa mwenyeji wa Atalanta BC kwenye mechi ya ligi ya Serie A ugani Stadio Giuseppe Meazza Mei 15.
 
Rossoneri emerged as 3-1 winners over Hellas Verona away in their previous league match which was played on May 15. Katika mechi ya ligi iliyochezwa Mei 8, Milan waliibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Hellas Verona wakiwa ugenini.
 
Ushindi huo uliendeleza msururu wa Milan bila kushindwa hadi mechi kumi na nne za ligi huku wakiandikisha ushindi kwenye mechi tisa na kupata sare tano.

Stefano Pioli
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Vile vile, Rossoneri hawajashindwa katika mechi saba za ligi zilizopita wakiwa nyumbani, wakiandikisha ushindi mara nne na sare tatu ugani Stadio Giuseppe Meazza.
 
"Nawapenda sana wachezaji wangu. Naelewa sana wanavyojituma tangu tumeanza safari hii pamoja,” alisema meneja wa Milan Stefano Pioli baada ya ushindi dhidi ya Verona.  
 
"Uzoefu unachangia sana kujiamini na ujasiri. Leo walitangulia kufunga japokuwa tulianza vizuri. Tunajiamini. Hatua baada ya hatua tunavuka changamoto zote.
 
"Tunafaa kuendelea hivi hivi. Nimefurahishwa na ushindi wa leo lakini tayari tunawaza kuhusu mechi ijayo ambayo tutakuwa nyumbani dhidi ya Atalanta Jumapili ijayo. Itakuwa mechi ngumu.”

Ruslan Malinovskyi
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwingineko, Atalanta wakiwa ugenini walipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Spezia kwenye mchezo wa ligi uliochezwa mnamo Mei 8.
 
Kwa sasa, Atalanta wameshinda mechi mbili na kupata sare mbili mfululizo katika mechi nne za ligi zilizopita.
 
Vile vile, Atalanta hawajashindwa katika mechi mbili zilizopita za ligi wakiwa ugenini huku wakipata ushindi katika mechi zote mbili hizo.
 
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya Milan na Atalanta ilikuwa mnamo Novemba 20 2021.
 
Milan walipata ushindi wa 3-2 dhidi ya Atalanta katika mechi hiyo iliyochezewa ugani 3-2 Gewiss Stadium ambao pia unajulikana kama Stadio Atleti Azzurri d'Italia.
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Milan - 2
Atalanta - 2
Sare - 1
 

Ratiba ya Serie A mchezo wa 37.

 
Mei 14 Jumamosi
 
4:00pm- Empoli FC v US Salernitana  
 
7:00pm- Hellas Verona v Torino FC 
 
7:00pm- Udinese Calcio v Spezia FC 
 
9:45pm- AS Roma v Venezia FC

 
Mei 15 Jumapili
 
13:30pm- Bologna FC v US Sassuolo 
 
4:00pm- SSC Napoli v Genoa CFC 
 
7:00pm- AC Milan v Atalanta BC 
 
9:45pm- Cagliari Calcio v Inter Milan 

 
Mei 16 Jumatatu
 
7:30pm- UC Sampdoria v ACF Fiorentina 
 
9:45pm- Juventus FC v SS Lazio 


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 05/12/2022