Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 UEFA Champions League
Semi-Final - Second-Leg
Real Madrid v Manchester City
Estadio Santiago Bernabeu
Madrid, Spain
Wednesday, 4 May 2022
Kick-Off 21h00 CAT
Real Madrid watakuwa mwenyeji wa Manchester City katika
mechi ya UEFA mkondo wa pili hawamu ya nusu fainali mnamo Mei 4.
Miamba hao wa soka wa Uhispania walishindwa na City 4-3 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza ugani Etihad Stadium nchini England Aprili 26.
Madrid hawajapata ushindi katika mechi mbili za mwisho za shindano hili huku wakishindwa kwenye mechi zote mbili na timu kutoka England, Chelsea FC na City.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
The Whites wataialika City ugani Estadio Santiago Bernabeu ambapo watakuwa na nia ya kufunga mabao mengi ili kufuzu kuingia fainali ya shindano hili.
Madrid walikuwa na msururu wa mechi tatu bila kushindwa wakiwa nyumbani katika shindano hili kabla ya Chelsea kuvunja msururu huo.
Mara ya mwisho Madrid kucheza mechi ya nusu fainali ya UEFA nyumbani ilikuwa msimu uliopita walipoialika Chelsea.
The Whites walipata sare ya1-1 katika mechi hio kabla ya kupata kichapo cha 2-0 ugenini dhidi ya Chelsea nchini England.
Chelsea walifuzu kuingia fainali ya shindano hilo na mwishowe kushinda taji hilo walipofunga Manchester City 1-0 kwenye fainali hiyo.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Inahuznisha kwa kiasi fulani kwa sababu hatukupambana vilivyo katika mechi hii hasa kipindi cha kwanza,” alisema Carlo Ancelotti baada ya timu yake kushindwa na City.
"Walifunga magoli mawili ambayo tungeyazuia vizuri iwapo tungekuwa na umakini. Tulipambana na tukafanikiwa kurudisha mabao matatu hivyo basi tuna nafasi kubwa katika mechi ya mkondo wa pili.
"Matokeo haya yanatupa nafasi nyingine kwenye mechi ya marudiano kwenye uwanja wa nyumbani Bernabeu. Tunatakiwa kuimarisha safu ya ulinzi kwa sababu tuna nguvu ya kutosha katika safu ya ushambuliaji na tutawatatiza kwenye mechi ya marudiano,” aliongeza.
"Ni muhimu sana kuimarisha safu yetu ya ulinzi kwenye mechi hiyo.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi za UEFA
Mechi - 7
Madrid - 2
City - 3
Sare - 2
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.