Djokovic Makini kuepuka Kushindwa na Bedene, Roland Garros


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 Roland Garros 

ATP Tour & WTA Tour 

Stade Roland Garros 
Paris, France
22 May - 5 June 2022
 
Novak Djokovic atakuwa makini kuepuka kushindwa na Aljaz Bedene kwenye mechi ya raundi ya tatu ya shindano la tenisi la Roland Garros 2022 Ijumaa hii.
 
Bingwa huyo mtetezi aliingia raundi ya tatu ya shindano la tenisi la French Open kwa kumshinda Alex Molcan wa Slovakia 6-2 6-3 7-6 katika mechi ya raundi ya pili iliyochezwa Jumanne.
 
Djokovic ambaye anashiriki shindano lake kubwa la kwanza mwaka huu, anatarajia kufika fainali na kutetea kwa mafanikio taji lake la Roland Garros, ambalo pia linajulikana kama French Open. 
Pablo-Cuevas.jpgHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Djokovic, ambaye ni mshindi mara mbili wa Roland Garros, alishinda shindano hili mwaka 2016 na 2021, na amesema kwamba kila kitu kinaenda vizuri baada ya kumshinda Molcan.
 
"Mambo yanaenda vizuri kwa sasa. Nafurahi ninavyojihisi ninapokuwa uwanjani nikicheza,” alisema Djokovic.
 
"Mazingira ya leo yamekuwa changamoto kwa kiwango fulani ukizingatia pia ilikuwa dhidi ya mpinzani aliye na uzoefu kwenye sakafu ya udongo.
 
"Haukuwa mchezo rahisi. Hata hivyo nadhani nilicheza vizuri. Kila jambo linaenda vizuri. Naisubiri changamoto itakayofuata.”
 
Kwingineko, Bedene alifuzu baada ya kumshinda mchezaji kutoka taifa la Uruguay Pablo Cuevas 4-6, 6-4, 7-6(5), 6-4 katika mechi ya raundi ya pili iliyochezwa Jumanne.
 
Bedene kutoka Slovenia aliingia raundi ya pili baada ya kumshinda Christopher Connell wa Australia kwenye mechi ya raundi ya kwanza Jumatatu.
 
Bedene ameshinda mashindano matano ya tenisi ya Futures na mashindano 14 ya mchezaji mmoja kila upande ya Challenger (shindano la ngazi ya chini ya ATP) na sasa anashikilia nafasi ya 195 katika jedwali rasmi la bodi ya tenisi duniani (ATP).
 
Hii itakuwa ni mara ya nne kwa Djokovic na Bedene kukutana katika shindano la ATP.
 
Djokovic ameshinda mara zote tatu alizokutana na Bedene.
 
Mchezaji huyo anayeshikilia nafasi ya kwanza duniani alimshinda Bedene 7-6(2), 6-2 mwaka 2017 kwenye shindano la tenisi la Italian Open katika mechi ya raundi ya pili ambayo ilikuwa ni mara yao ya mwisho kukutana.
 

Djokovic vs Bedene 

Takwimu baina yao katika mashindano yote ya ATP. 

Djokovic - 3
Bedene - 0


Bashiri tenisi mtandaoni

Bashiri manguli kwenye michuano bora ya tenisi kutoka Wimbledon hadi Roland Garros. Jisajili leo na anza kubashiri kwenye machaguo tofauti ambayo tenisi inakupatia; kutoka 1x2 matokeo ya mechi, bashiri kwa mchezaji wako unayempenda hadi kwenye bashiri nyingi kama Mshindi wa Set. Chochote unachochagua kufanya, Betway ina chaguo kwaajili yako.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway
 
 

Published: 05/27/2022