City watarajia kuendeleza ubabe dhidi ya Hammers


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English Premier League

Matchday 37

West Ham United v Manchester City

London Stadium
London, England
Sunday, 15 May 2022
Kick-off is at 16h00  
 
Manchester City watakuwa mgeni wa West Ham United ugani London stadium katika mechi ya premier mnamo Mei 15 jumapili wakiwa na nia ya kutetea taji hilo.
 
The Citizens waliongeza nafasi kati yao na Liverpool hadi alama tatu walipoishinda Newcastle 5-0 Etihad Stadium wikendi iliyopita baada ya Liverpool kupata sare ya 1-1 dhidi ya Tottenham.
 
Timu ya Pep Guardiola imefanikiwa kufunga mabao 17 kwenye mechi nne zilizopita na kuruhusu goli moja tu.  

Pep Guardiola
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Guardiola alikisifia kikosi chake baada ya ushindi dhidi ya the Magpies kwa ukakamavu kilichoonyesha tangu aliporidhi mikoba ya kukinoa.
 
"Wakati mwingine nawashauri wachezaji kucheza vizuri ili kuwafurahisha mashabiki na kutoa ujumbe kwa timu pinzani kuwa hii sio sehemu salama kuja,” alisema raia huyo wa Uhispania.
 
"Hatukuhitaji kufanya hivyo leo kwa sababu mashabiki wanafahamu kuwa wachezaji hawa wamekuwa wakicheza hivyo kila baada ya siku tatu kwa miaka mitano. Ni moja kati ya kikosi kizuri nilichowai kuwa nacho kama kocha na pia mchezaji.
 
"Ni alama tatu muhimu hasa baada ya Liverpool kupata sare ya 0-0 na Tottenham lakini chochote chaweza kutokea kwenye soka.”
 
The Hammers waliimarisha nafasi ya kucheza mechi ya Ulaya kwa kuishinda 4-0 Norwich, ambao tayari wameshuka daraja ugani Carrow Road, wikendi iliyopita.
 
Hapo awali, nafasi ya West Ham kuingia nafasi ya kucheza mechi za Ulaya ilionekana finyu baada ya kushinda mechi tano kati ya tisa lakini baada ya ushindi huo, sasa wapo nafasi ya saba na alama tano zaidi ya Wolves.

David Moyes
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Vijana wa David Moyes waliondolewa kwenye ligi ya Europa msimu huu na Eintracht Frankfurt mapema wiki hii katika hatua ya nusu fainali na ushindi dhidi ya Norwich uliwapa motisha.
 
"Kuondolewa kwenye ligi ya Europa kulituvunja moyo sana. Ushindi wa leo umetupa motisha,” alisema Moyes.
 
"Ukweli ni kuwa tunahitaji kucheza mechi za ulaya tena. Tunapambana sana kuafikia hilo. Ushindi wa leo ulikuwa muhimu sana ukizingatia kuwa zimesalia mechi mbili tu ambazo ni ngumu.
 
"Alama tatu za leo zitatupa matumaini kuipita Manchester United na kuwaacha Wolvehampton Wanderers. Ni muhimu sana.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi

Mechi - 5
West Ham - 0
Man City - 4
Sare - 1


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 05/10/2022