Blues na Reds kwenye fainali ya FA Wembley


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English FA Cup

Final

Chelsea v Liverpool

Wembley Stadium
London, England
Saturday, 14 May 2022
Kick-off is at 18h45 
 
Chelsea na Liverpool watakutana kwenye mechi ya fainali ya kombe la FA ugani Wembley Jumamosi Mei 14. Hii ni miezi mitatu iliyopita baada ya timu hizi kukutana kwenye fainali ya kombe la EFL. 
 
The Reds waliibuka na ushindi kwenye fainali ya EFL baada ya kuishinda Chelsea kwa njia ya matuta ya penalti (11-10) ugani Wembley mwezi Februari. Mechi iliisha sare ya 0-0 kwenye muda wa kawaida na ziada. 
 
Vile vile, mechi mbili za ligi baina ya timu hizi mbili msimu huu zimeishia sare ya 1-1 ugani Anfield mwezi Januari na 2-2 ugani Stamford Bridge mwezi Agosti. 
 
Chelsea walishinda Chesterfield, Plymouth, Luton, Middlesbrough na Crystal Palace kwenye safari ya kufika fainali yao ya 16, ikiwa wameshinda mashindano haya mara nane, mara ya mwisho dhidi ya Manchester United mwaka 2018 (1-0)

Ruben Loftus-Cheek
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Ruben Loftus-Cheek ambaye alifunga bao la kwanza dhidi ya Crystal Palace na ambalo likiwa ni goli lake la kwanza kwa Chelsea ndani ya muda wa miaka mitatu anatazamia kulipa kisasi dhidi ya Liverpool. 
 
"Tunataka kulipiza kisasi. Ndio mpango wetu. Ulikuwa mchezo mzuri kwenye fainali iliyopita. Yeyote angeweza kupata ushindi. Tunalifahamu hilo na tunataka kupata ushindi dhidi yao,” Loftus-Cheek alisema. 
 
"Siku zote nataka kushinda mataji na kusaidia timu yangu kwa kiwango kikubwa. Nahisi kwamba nimecheza sana kwenye mechi za kombe hili, chochote kinaweza kutokea siku ya fainali lakini nitakuwa tayari.” 
 
Kwengineko, Liverpool iliwaondoa Shrewsbury, Cardiff, Norwich, Nottingham Forest na Manchester City ili kuingia fainali yao ya 15 ambayo ni ya kwanza tangu walipopoteza 2-1 dhidi ya Chelsea miaka kumi iliyopita. 

Alisson Becker
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Alisson aliokoa mikwaju kadhaa dhidi ya City kwenye mechi ya nusu-fainali na kuweka hai matumaini ya Liverpool kushinda mataji manne. Raia huyo wa Brazil ana hamu sana ya kucheza kwenye fainali ya shindano hilo ambalo ni la zamani zaidi kuliko yote kisoka duniani. 
 
"Soka ni mojawapo ya njia za kutengeneza kumbukumbu. Inafurahisha sana kuwa na uwezo wa kuafikia malengo na kushinda mataji,” 
 
"Tunajaribu kila siku kufanikisha malengo yetu kwa kujiandaa ipasavyo ili kuwa na uwezo wa kupambana uwanjani na kuisaidia Liverpool kushinda na kushinda tena mataji yote ambayo tunashindania. Hilo ndilo lengo letu.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi za FA

Mechi - 11
Chelsea - 7
Liverpool - 4
Sare - 0

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 05/13/2022