Barcelona watamani ushindi dhidi Celta


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Spanish La Liga

Matchday 36

FC Barcelona v Celta Vigo

Camp Nou
Barcelona, Spain 
Tuesday, 10 May 2022
Kick-off is at 21h30  
 
FC Barcelona watamwalika Celta Vigo katika mechi ya ligi kuu ya Uhispania ugani Camp Nou Mei 10.
 
Hii itakuwa ni mara ya 50 ya timu hizi kukutana katika mashindano yote tangu msimu 1993/94 
 
Barcelona ameshinda mechi 24 kati ya mechi hizo 50, Celta Vigo akashinda 11 huku timu hizo zikitoa sare mara 14. 

Sergi Roberto
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Mara ya mwisho timu hizi kukutana katika mechi ya ligi ilikuwa Novemba 6 2021 ambapo Celta walilazimisha sare ya 3-3 ugani Estadio Municipal de BalaĆ­dos.
 
Barcelona wamekuwa na matokeo mseto katika mechi za nyumbani Camp Nou ingawaje walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Real Mallorca katika mechi ya mwisho nyumbani tarehe 1 Mei. 
 
Kabla ya mechi dhidi ya Real Mallorca, Barcelona walikuwa wamecheza mechi mbili za awali nyumbani bila ushindi.
 
Kwingineko, Celta wamekuwa wakipata matokeo mazuri ugenini huku mechi ya mwisho wakipata sare ya 1-1 dhidi ya Granada CF katika mechi ya ligi ya Mei 1. 

Eduardo Coudet
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Katika mechi mbili zilizopita ugenini, Celta Vigo wameshinda mechi moja ambayo ilikuwa dhidi ya Athletic Bilbao na kupata sare kwenye mechi ya pili. 
 
"Lengo letu lilikuwa kupata alama zote tatu,” alisema meneja wa Celta Vigo Eduardo Coudet baada ya Sare dhidi ya Granada. 
 
"Tulitengeneza nafasi nne za wazi kipindi cha kwanza na nyingine nne au tano za kumaliza mchezo lakini hatukufunga mabao. Tumeadhibiwa kwa kutowajibika. 
 
"Granada hawakutengeneza nafasi kama tulivyofanya sisi lakini tulikosa umakini katika ufungaji. Tumepoteza alama mbili muhimu tulizozihitaji dhidi ya mpinzani mkubwa kwetu,” aliongeza. 
 
"Tulifanya kila tuwezalo kupata ushindi na alama tatu lakini mpinzani wetu alijikakamua na kufunga bao la kusawazisha kwa sababu hatukuwa na umakini katika kudhibiti mchezo.” 
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi

Mechi - 5
Barcelona - 2
Celta - 1
Sare - 2
 

Ratiba ya La Liga mchezo wa 36

 

Majira ya Afrika ya kati.

 
Mei 10 Jumanne
 
7:00pm- Valencia CF v Real Betis 
 
8:00pm- Granada CF v Athletic Bilbao 
 
9:30pm- FC Barcelona v Celta Vigo 

 
Mei 11 Jumatano
 
7:00pm- Deportivo Alaves v RCD Espanyol
 
7:00pm- CA Osasuna v Getafe CF
 
8:30pm- Sevilla FC v Real Mallorca 
 
9:30pm- Elche CF v Atletico Madrid 

 
Mei 12 Alhamisi
 
7:00pm- Real Sociedad v Cadiz CF 
 
8:00pm- Rayo Vallecano v Villarreal CF  


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 05/09/2022