Bagnaia apania ushindi wa pili mfululizo French MotoGP


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 MotoGP Season

French Grand Prix

Round 7 
Circuit Bugatti
Le Mans, France
Sunday, 15 May 2022

Francesco Bagnaia anapania kupata ushindi wa pili mfululizo katika mbio za pikipiki za French MotoGP msimu 2022 atakaposhiriki mbio hizo Mei 15.
 
Mwendeshaji huyo wa Ducati alikosa nafasi ya jukwaa kwenye mbio za French MotoGP mwaka jana kwa alama ndogo baada ya kumaliza katika nafasi ya nne.
 
Bagnaia alishinda mbio za pikipiki za Spanish MotoGP mnamo Mei 1 ambazo ni mbio za hivi karibuni za msimu 2022 wa MotoGP na kujiweka katika nafasi nzuri ya kupigania taji.
 
Aleix Espargaro of Aprilia Racing
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Ulikuwa ni ushindi wa kwanza wa raia huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 25 msimu huu baada ya kumaliza katika nafasi ya tano kwenye mbio mbili mfululizo.
 
Bagnaia alifuatiwa na mwendeshaji wa Yamaha Fabio Quartararo huku Aleix Espargaró wa Aprilia akimaliza katika nafasi kwenye mbio za Spanish MotoGP.
 
Bingwa mtetezi wa dunia wa mbio za pikipiki Quartararo anashikilia nafasi ya kwanza kwenye jedwali la waendeshaji akifuatiwa na Espargaróhuku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Enea Bastianini wa Ducati.
 
Bagnaia ambaye ni bingwa wa MotoGP wa dunia wa mwaka 2018 anashikilia nafasi ya tano na uenda akaingia nafasi za kwanza tatu iwapo atashinda mbio za mkondo wa Circuit Bugatti. 

Fabio Quartararo
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
“Ni siku nzuri. Tulihangaika sana kwenye mbio za majaribio lakini tuliendelea kujikaza,” alisema Bagnaia baada ya ushindi wa Spanish MotoGP.
 
“Tulifanya vizuri wikendi hii. Nafurahi sana kwa sababu tumerudi katika ubora wetu.”
 
“Nilikuwa na bahati kushiriki mbio za Ureno,” aliongeza Bagnaia ambaye alimaliza kwenye nafasi ya nane katika mbio za Portuguese MotoGP Aprili 24.
 
“Mwaka jana Fabio alifanya vizuri sana kwenye mkondo huu lakini leo tumefanya kazi nzuri zaidi.”
 
Ducati wanashikilia nafasi ya kwanza kwenye jedwali la waundaji, wakifuatiwa na Yamaha na Aprilia mtawalia.
 

Matokeo ya French Grand Prix 2021

 
Mshindi: Jack Miller- Ducati
Nafasi ya pili: Johann Zarco - Ducati
Nafasi ya tatu: Fabio Quartararo - Yamaha
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 05/12/2022