Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo
BEKI wa kazi Wilson Nangu miongoni mwa wachezaji ambao wanavuja jasho ndani ya JKT Tanzania ambayo ipo ndani ya 10 bora anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Kariakoo ambao ni
Simba na Yanga wote wakiwa katika hesabu za kuinasa saini yake.
Ipo wazi kuwa katika eneo ambalo JKT Tanzania haijawa imara sana ni eneo la ushambuliaji ikiwa na wastani mdogo katika kucheka na nyavu baada ya mechi 21 safu ya ushambuliaji imefunga mabao 15 msimu wa 2024/25.
Eneo ambalo imekuwa imara ni eneo la ulinzi ikiwa ndani ya timu tano bora ambazo zimefungwa mabao machache, JKT Tanzania ni namba tano ikiwa imefungwa mabao 15 ndani ya mechi 21.
Ndani ya dakika 1,890 ni mabao 15 imefungwa ikiwa na wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 126 huku ikiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 126 uwanjani.
Ni timu ya kwanza kuambulia sare mbele ya Yanga baada ya ubao wa Meja Isamuhyo Februari 10 2025 kusoma JKT Tanzania 0-0 Yanga na mchezaji bora alikuwa ni Nangu.
Rekodi zinaonyesha kuwa Nangu aliokoa hatari zaidi ya 5 miongoni mwa hizo ilikuwa dakika ya 44, 45, 55, 68, 69, 73, 83, 90. Alicheza faulo ya hatari dakika ya 69 ikawa chanzo kwake kuonyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Ahmed Arajiga.
Alianza kikosi cha kwanza Februari 13 2025 wakati wakipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars alianza kikiso cha kwanza pia kwenye mchezo dhidi ya KMC wakati wakipata ushindi wa mabao 2-0 Uwanja wa KMC Complex.
Nyota huyo anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Kariakoo ambao wanamfuatilia ndani ya msimu kuona namna kasi yake inavyokuwa uwanjani ili kupata saini yake.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.