MNARA WA CHAMA WAANZA KUSOMA SIMBA...


Kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amezidi kuimarisha namba zake katika Ligi Kuu Bara baada ya juzi usiku kufunga mabao mawili yaliyoizamisha Mashujaa kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex na kumfanya sasa afikishe jumla ya mabao sita kwa msimu huu.
 
Tangu Ligi Kuu iliporejea mapema mwezi uliopita baada ya kusimama kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 na Fainali za Afcon 2023, Simba imecheza mechi tisa na Chama ameifungia mabao manne, yakiwamo mawili ya juzi na kumfanya kuhusika na mbao 11 hadi sasa kwani ameasisti pia mara tano.
 
Msimu uliopita nyota huyo wa kimataifa wa Zambia, alifunga mabao manne tu, japo aliongoza kwa asisti akitoa pasi za mabao 15 na kumfanya msimu mzima kuhusika na mabao 19, ikiwa ni manane zaidi na aliyohusika nayo hadi sasa huku Simba ikiwa imecheza mechi 19 na kusaliwa na 11 kibindoni.
 
Katika mechi ya juzi, Chama alifunga bao la kwanza dakika ya 57 akimalizia pasi tamu ya kutoka pembeni iliyopigwa na Willy Onana aliyepokea awali mpira wa kurushwa na Mzambia huyo kupiga ‘muwa’ ulioenda kugonga juu ya lango kabla ya kutumbukia wavuni na kuongeza la ;pili dakika ya 73 akimalizia pasi ya upendo kutokwa kwa nahodha msaidizi, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, aliyefikisha asisti ya nne msimu huu.
 
Chama aliyekuwa amesimamishwa na uongozi kwa tuhuma za utovu wa nidhamu sambamba na kiungo Nassor Kapama aliyepo Mtibwa Sugar kwa sasa, tangu amerejea kwenye fainali za Afcon 2023 alipoenda na timu ya taifa ya Zambia na kuishia makundi, amekuwa na kiwango cha hali ya juu na kuipa Simba pointi saba katika mechi tatu alizofunga.
 
Chama alifunga katika mechi ya sare ya 1-1 dhidi ya Azam FC, kisha akafunga bao pekee mbele ya JKT Tanzania na juzi tena akatupia mawili, mbali na asisti tatu alizotoa kwenye mechi ambazo Simba ilitoka na ushindi dhidi ya Tabora United na Coastal Union, pia akifunga bao moja na kuasisti moja wakati Suimba ikiifumua Jwaneng Galaxy ya Botswana katika Ligi ya Mabingwa Afrika, ushindi ulioivusha Simba kuingia robo fainali na sasa itacheza na Al Ahly.
 
Kiungo huyo, aliwahi kunukuliwa akisema kwamba anafurahia kuisaidia timu kupata matokeo ya ushindi kama hajafuinga basi hujitahidi aasisti na kwamba ndio kazi iliyomleta Msimbazi na anapenda kuwapa furaha mashabiki.
 
Chama anaenda timu ya taifa ya Zambia kabla ya kurejea kuungana na wenzke kwa ajili ya mechi ya kwanza ya robo fainali itakayopigwa Machi 29 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kisha kurudiana nao Cairo April 6.


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 03/25/2024