KIUNGO wa
Simba, Ladack Chasambi amesema siri kubwa anayoambiwa na Kocha Abdelhak Benchikha anamuamini anatakiwa kupambana na kufuata yale aliyompa katika uwanja wa mazoezi.
Amesema amekuwa akimsisitiza kujitoa kwa ajili ya timu hali ambayo amekuwa na kiwango bora na kufanikiwa kuwa miongoni mwa wachezaji walifunga mabao 6-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
Nyota huyo aliyesajiliwa kipindi cha dirisha dogo akitokea Mtibwa Sugar juzi alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akiingia katika kipindi cha pili na kufanikiwa kufunga bao lake la kwanza katika michuano hiyo
Chasambi amesema anafurahi kuwa miongoni mwa wachezaji walioingia katika historia kubwa ya kuipeleka Simba robo fainali ikiwa kwake ndio mara ya kwanza.
Amesema siri kubwa ya kuendelea kuonyesha uwezo mkubwa ni kufuata maelekezo ya benchi la ufundi ambapo Kocha Benchikha akimuamini na kumtaka kufanya vizuri kila anapompa nafasi.
“Kocha amekuwa anaamini kila uwezo wa mchezaji ndani ya hii timu, amekuwa akinieleza juu ya uvimilivu lakini kutaka kuniona najitoa, napambama kila anaponipa nafasi ya kucheza na kufuata yale anbayo amekuwa akielekeza,” amesema Chasambi.
Ameongeza kuwa amekuwa akifanya hivyo hali ya mechi ya FA dhidi ya TRA FC alifunga lakini kikubwa kwake kucheza mechi kubwa na kufunga jambo ambalo limeingia katika Historia ya maisha yake.
“Ni kweli kuna changamoto ya namba lakini sina hofu juu ya ujio wangu Simba kwa sababu kocha anatoa nafasi na ninaimani nitaendelea kupambana na sitamuangusha kwa maamuzi yake,” amesema Chasambi.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.