UCL - Real Madrid v Liverpool


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 UEFA Champions League

Round of 16
Second leg

Real Madrid v Liverpool

Estadio Santiago Bernabeu
Madrid, Spain
Wednesday, 15 March 2023
Kick-off is at 23h00  
 
Real Madrid wamekuwa na matokeo mseto katika mechi za hivi karibuni na Liverpool wanatariajia kuongeza machungu zaidi watakapokutana nao kwenye mechi ya mkondo wa pili ya roundi ya 16 ya UEFA ugani Bernabeu Jumatano Machi 15.
 
Los Blancos walitoka nyuma magoli mawili na kushinda 5-2 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza ugani Anfield Februari 21.
 
Vijana wa Carlo Ancelotti hawajashinda mechi yoyote tangu muda huo huku wakipata sare ya 1-1 dhidi ya Atletico Madrid na Real Betis (0-0) kwenye mechi za La liga kabla ya kupoteza 1-0 mechi ya nusu fainali ya Copa del Rey dhidi ya Barcelona. 
 
Vinicius Junior
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Kwingineko, the Reds hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika mechi tatu zilizopita tangu walipocheza na Madrid mwezi uliopita huku wakipata sare Crystal Palace (0-0) na kuichapa Wolves 2-0 na kisha kuigaragaza Manchester United 7-0. 
 
Timu ya Jurgen Klopp sasa ipo nyuma ya Tottenham na alama tatu tu wakiwa na mechi moja mkononi huku wakipania kumaliza katika nafasi nne bora mwishoni mwa msimu. 
 
Mchezaji Vinicius Junior alifungia Madrid goli la kwanza dhidi ya Liverpool na kisha kufunga la pili huku akionekana kuwa na bahati ya kufungu katika shindano hili baada ya kufunga magoli manne katika mechi tatu zilizopita. Mchezaji huyo raia wa Brazil ndiye mfungaji bora wa Madrid katika shindano hili msimu huu akiwa na magoli sita kutokana na jumla ya mechi saba. 
 
Mohamed Salah hajawa akifunga magoli sana kwenye ligi msimu huu ila takwimu zake za ufungaji katika UEFA zinaashiria hali tofauti. Amefanikiwa kufunga magoli nane kutokana na mechi saba na kumweka kileleni cha wafungaji bora wa shindano hili msimu huu. Raia huyo wa Misri alifunga magoli matatu ya haraka maarufu kama hat-trick ya shindano hili alipoingia kama mchezaji wa akiba dhidi ya Rangers na kufunga magoli hayo kwa muda wa dakika sita tu kwenye hatua ya makundi. 

Mo Salah
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Katika habari ya vikosi, wenyeji Madrid watakosa wachezaji Andriy Lunin na David Alaba  huku Calvin Ramsay, Luis Diaz Thiago Alcantara, Joe Gomez, Naby Keita na Arthur Melo wakikosa mechi hiyo kwa upande wa Liverpool.
 
Ancelotti anasisitiza kwamba bado wana kibarua kigumu mbele yao na kwamba kazi haijaisha kwani Liverpool ni hatari. 
 
"Tumepata matokeo katika dakika za kwanza tisini na sasa kazi kubwa ni kulinda ushindi huo,” alisema. “Liverpool wana ushindani mkubwa hivyo basi mechi hii haijakamilika. 
 
"Liverpool ni timu nzuri kwa sababu wanacheza kwa kasi sana jambo ambalo ni nadra sana kwenye mechi za UEFA. Hautakuwa mchezo rahisi kwetu.” 
 
Klopp anakiri kuwa timu yake italazimika kujituma zaidi ili kubadilisha matokeo hayo ila anasema hawawezi kufanya hivyo bila tahadhari kwa sababu Madrid wanafahamika kwa mashambulizi yao ya kushtukiza.
 
"Ukiangalia matokeo ya leo 5-2 utagundua kuwa ni wazoefu wa mashambulizi ya kushtukiza. Tunahitajika kufunga magoli matatu ugenini na hilo halitakuwa rahisi,” alisema. 
 
"Tutakwenda huko tukiwa na lengo la kushinda mechi. Iwapo itawezekana au la sina hakika ila tutajaribu sana kushinda mechi hiyo.” 
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za UEFA. 

Mechi - 5
Real Madrid - 4
Liverpool - 0
Sare - 1
 

Ratiba ya mechi za UEFA:

 
Machi 14 Jumanne
 
11:00pm: Manchester City v RB Leipzig
 
11:00pm: Porto v Inter Milan
 
Machi 15 Jumatano
 
11:00pm: Real Madrid v Liverpool
 
11:00pm: Napoli v Eintracht Frankfurt


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 03/14/2023