Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 UEFA Champions League
Round of 16 - Second-Leg
Bayern Munich v Paris Saint Germain
Allianz Arena
Münch, Germany
Wednesday, 8 March 2023
Kick-off is at 22h00
Bayern Munich watakuwa mwenyeji wa Paris Saint-Germain ugani Allianz Arena Machi 8 kwa ajili ya mechi ya
ligi ya klabu bingwa ulaya (UEFA)
Matokeo yao kwenye mechi za UEFA
Mabingwa hao wa ligi ya Ujerumani waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi PSG kwenye mechi ya mkondo wa kwanza nchini Ufaransa Februari 14.
Bayern hawajapoteza mechi ya UEFA katika michezo nane iliyopita huku wakishinda mechi saba mfululizo na kutoa sare moja.
Vile vile, The Bavarians hawajapoteza mechi ya UEFA katika mechi nane za mwisho wakiwa nyumbani baada ya kuandikisha ushindi kwenye mechi hizo nane mfululizo.
Msururu wa mechi sita katika shindano hili bila kushindwa kwa upande wa PSG ulifika kikomo walipopoteza dhidi ya Bayern. Kabla ya mechi hiyo, PSG walikuwa wameshinda mechi nne na kupoteza mechi mbili.
Hata hivyo, mabingwa hao wa Ufaransa hawajashindwa katika michezo mitatu ya shindano hili wakiwa ugenini wakiandikisha ushindi wa mechi mbili na kupata sare moja.
Athari ya matokeo ya mechi hii.
Bayern watafuzu kuingia hatua ya robo fainali ya shindano hili iwapo wataepuka kushindwa na PSG huku droo ya robo fainali ikitarajiwa kuandaliwa Machi 17.
PSG watahitaji kushinda mechi hiyo kwa magoli mawili zaidi ili kuwa na nafasi ya kuingia hatua ya robo fainali. Ushindi wa goli moja zaidi utapeleka mechi hiyo kwenye muda wa ziada.
Vikosi.
Lucas Hernández, Manuel Neuer na Noussair Mazraoui watakosa mechi hiyo kutokana na majeraha ilhali mlinzi Benjamin Pavard atakosa mechi hiyo kutokana na marufuku.
PSG watakosa huduma za wachezaji wa kikosi cha kwanza; Presnel Kimpembe, Renato Sanches, Achraf Hakimi pamoja na Neymar ambao wanauguza majeraha.
Wachezaji wa kutegemewa
Bayern Munich wataweka matumaini kwa mchezaji Leroy Sane ambaye tayari amefunga magoli manne kwenye shindano hili msimu huu.
Baada ya kufunga magoli saba katika shindano hili msimu huu, Kylian Mbappe atakuwa na jukumu kubwa mbele yake kuhakikisha PSG wanafuzu hatua ya robo fainali.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Nukuu
"Naelewa sana uchungu wa mashabiki wetu. Tutahitaji kuongeza juhudi na kushambulia zaidi kwenye mechi ya marudiano,” alisema mlinzi wa PSG Sergio Ramos baada ya kupoteza dhidi ya Bayern.
"Tunataka kupata ushindi na kucheza mchezo mzuri. Chochote kinaweza kutokea katika mchezo wa soka. Wakati mwingine tunacheza mchezo mzuri na wakati mwingine hatuna mchezo mzuri. Cha msingi ni matokeo ya mwisho.
"Kadri tunavyocheza ndivyo uzoevu unaongezeka na tutazidi kuimarika mechi baada ya mechi.”
Takwimu baina ya timu hizi.
Bayern walipoteza 3-2 kwenye mechi ya mwisho walipowaalika PSG ugani Allianz Arena mnamo Aprili 7 2021.
Hata hivyo, Bayern wanaelekea kwenye mchezo huu wa Machi 8 ikiwa hawajapoteza mechi dhidi ya PSG katika michezo miwili iliyopita.
(Takwimu baina ya timu hizi katika mehi za UEFA)
Mechi - 12
PSG - 6
Bayern - 6
Sare - 0
Ratiba ya mechi za UEFA – Tarehe 7 na 8 Machi
Mechi zote zitaanza 10:00pm
Machi 7 Jumanne
Chelsea FC v Borussia Dortmund
SL Benfica v Club Brugge
Machi 8 Jumatano
Bayern Munich v Paris Saint-Germain
Tottenham Hotspur v AC Milan
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.