NBA: Los Angeles Lakers v Toronto Raptors 


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 National Basketball Association (NBA) season

Regular Season

Los Angeles Lakers v Toronto Raptors 

Crypto.com Arena
Los Angeles, USA
Saturday, 11 March 2023 
05h30  
 
Los Angeles Lakers watamenyana na Toronto Raptors kwenye mechi ya ligi ya mpira wa kikapu National Basketball Association (NBA) Machi 5.
 
Takwimu baina ya timu hizi
 
Timu hizi zitakuwa zinakutana kwa mara ya 53 kwenye mechi za ligi tangu mwaka 1995 timu ya Raptors ilipoasisiwa.
 
The Lakers umeonyesha ubabe wao kwenye mechi baina ya Raptors kwani wamefanikiwa kushinda mechi 30 ukilinganisha na mechi 22 kwa faida ya Raptors katika mechi 52.
 
Mechi ya mwisho baina yao.  
 
The Raptors walipata ushindi wa 126-113 dhidi ya Lakers mnamo Desemba 8 2022 ambapo mchezaji Pascal Siakam alichangia alama 25 kwenye mechi hiyo.
 
Mchezo baina ya timu hizi ulifanyika katika ukumbi wa Scotiabank Arena.
 
Athari za matokeo ya mechi hii.
 
The Lakers bado wana matumaini ya kufuzu kucheza mechi za mchujo kwani wapo katika nafasi ya 11 kwenye michezo ya Western Conference baada ya kuandikisha ushindi mara 31 na kupoteza mechi 34.  
 
Kwa upande mwingine, matumaini ya Raptors kushiriki mechi za mchujo bado yapo kwani wapo katika nafasi ya tisa kwenye michezo ya Eastern Conference baada ya kushinda mechi 32 na kupoteza 34.
 
Wachezaji muhimu
 
Russell Westbrook ni mmoja wa wachezaji mahiri kwa upande wa Los Angeles Lakers na alichangia alama 16 na kuchangia nyingine tatu mnamo Desemba walipopoteza dhidi ya Raptors.
 
Fred VanVleet alichangia alama 25 na kusaidia nyingine saba Raptors walipoishinda Lakers na anatazamiwa kuwa na ushawishi mkubwa kwenye mechi ya marudiano.
 
Nukuu
 
Denver Nuggets walipata ushindi wa 118-113 dhidi ya Raptors Jumanne Machi 7 2023 katika ukumbi wa Ball Arena.
 
Akizungumzia mechi hiyo, kocha mkuu wa Raptors Nick Nurse alisema kuwa mchezo walioonyesha usiku huo ungeweza kuwapa ushindi kwenye mechi nyingine.
 
“Tukicheza kama tulivyocheza leo pengine tunaweza kumshinda yeyote,” alisema kocha huyo bora wa mwaka 2020.
 
“Tulicheza vizuri na kuwadhidbiti katika kila sekta lakini mwishowe hatukuweza kupata ushindi.”
 
Ratiba ya mechi za NBA – tarehe 11 na 12 Machi

Machi 11 Jumamosi


03:00am - Philadelphia 76ers v Portland Trail Blazers
03:00am - Washington Wizards v Atlanta Hawks
04:00am - Miami Heat v Cleveland Cavaliers
04:00am - Minnesota Timberwolves v Brooklyn Nets
04:00am - San Antonio Spurs v Denver Nuggets
06:30am - Los Angeles Lakers v Toronto Raptors
12:00pm - Los Angeles Clippers v New York Knicks

Machi 12 Jumapili

03:00am - Charlotte Hornets v Utah Jazz
03:00am - Detroit Pistons v Indiana Pacers
03:00am - Orlando Magic v Miami Heat
03:30am - Atlanta Hawks v Boston Celtics
04:00am - Houston Rockets v Chicago Bulls
04:00am - Memphis Grizzlies v Dallas Mavericks
04:30am - Golden State Warriors v Milwaukee Bucks
04:30am - New Orleans Pelicans v Oklahoma City Thunder
05:00am - Phoenix Suns v Sacramento Kings
10:30pm - Denver Nuggets v Brooklyn Nets
12:00pm - Charlotte Hornets v Cleveland Cavaliers
 

Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.




Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 03/10/2023