Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 Spanish La Liga
Matchday 27
Real Madrid v Real Valladolid
Estadio Santiago Bernabéu
Madrid, Spain
Sunday, 2 April 2023
Kick-off is at 16h15
Real Madrid na Real Valladolid watamenyana vikali kwenye mechi ya
ligi kuu Uhispania ugani Estadio Santiago Bernabéu Aprili 2 wakiwa na lengo la kutetea taji hilo.
Matokeo ya hivi karibuni
The Whites walipoteza 2-1 ugenini dhidi ya FC Barcelona mnamo Machi 19 na kufikisha kikomo msururu wa mechi tano za ligi bila kushindwa.
Hata hivyo, Madrid hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika michezo 16 iliyopita wakiwa nyumbani huku wakiandikisha sare 5 na kushinda mechi 11 ugani Estadio Santiago Bernabéu.
Kwa upande mwingine, Valladolid walipoteza 3-1 nyumbani mikononi mwa Athletic Bilbao mnamo Machi 17, ikiwa ni mechi ya pili mfululizo bila ushindi kwenye ligi.
Vile vile, The White and Violets hawana ushindi wowote katika mechi tatu za ligi zilizopita wakiwa ugenini baada ya kuandikisha sare moja na kushindwa mechi mbili mfululizo.
Athari ya matokeo ya mechi hii.
Madrid wanashikilia nafasi ya pili kwenye ligi wakiwa alama 12 nyuma ya viongozi wa ligi Barcelona. Wanahitaji ushindi ili kuweka hai ndoto ya kushinda taji la ligi.
Madrid ambao ni mabingwa watetezi wanatarajia kupata ushindi na kuweka hai matumaini ya kutetea taji hilo.
Valladolid wapo katika nafasi ya 16, alama 2 juu ya nafasi za kushuka daraja na ushindi kwenye mechi hii utawapa nafasi zaidi ya kusalia kwenye ligi.
Habari ya vikosi.
Ferland Mendy na Thibaut Courtois ni wachezaji tu wanaokosekana kwenye kambi ya Carlo Ancelotti kwa sasa. Hakuna mchezaji anayetumikia marufuku kwa upande wa Madrid.
Kama ilivyo kwa Madrid, Valladolid hawana mchezaji anayetumikia marufuku japokuwa wachezaji Anuar, Jordi Masip na Gonzalo Plata wanauguza majeraha.
Wachezaji muhimu
Madrid wanamtegemea sana mshambuliaji Karim Benzema kwenye mechi hii dhidi ya Valladolid kwani raia huyo wa Ufaransa amefanikiwa kufunga magoli 11 na kusaidia kupatikana kwa mengine 3 msimu huu.
Cyle Larin ni mchezaji wa kutegemewa kwa upande wa Valladolid. Nyota huyo amefunga magoli 5 katika mechi 8 za ligi tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka huu Januari.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Nukuu
“Tulikuwa na mchezo mzuri na tulistahili ushindi. Tuna maswali kuhusu goli lililokataliwa,” alisema Ancelotti baada ya kupoteza dhidi ya Barcelona.
"Tuliamini kuwa tulikuwa na ushindi tayari. Baada ya mchezo huu, tuna imani kuwa uwezo tunao kumaliza msimu huu vyema.”
“Hatukupata alama tatu kutokana na goli letu kukataliwa. Tuna mashaka na maamuzi hayo. Katika kombe la dunia, maamuzi ya mchezaji kuotea yalikuwa wazi kabisa ila hapa nina mashaka.”
Takwimu baina ya timu hizi.
Madrid walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Valladolid walipokutana mara ya mwisho kwenye ligi ugani Estadio José Zorrilla Desemba 30 2022.
Madrid hawajapoteza mchezo wa ligi dhidi ya Valladolid katika michezo 14 iliyopita huku wakiandikisha sare mbili na kushinda mechi 12.
Ratiba ya mechi za La liga - Machi 31- Aprili 3
Machi 31 Ijumaa
10:00pm- Real Mallorca v CA Osasuna
Aprili 1 Jumamosi
3:00pm - Girona FC v RCD Espanyol
5:15pm - Athletic Bilbao v Getafe CF
7:30pm - Cadiz CF v Sevilla FC
10:00pm- Elche CF v FC Barcelona
Aprili 2 Jumapili
3:00pm - Celta Vigo v UD Almeria
5:15pm - Real Madrid v Real Valladolid
7:30pm - Villarreal CF v Real Sociedad
10:00pm- Atletico Madrid v Real Betis
Aprili 3 Jumatatu
10:00pm - Valencia CF v Rayo Vallecano
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.