EPL - Manchester City v Liverpool


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 29

Manchester City v Liverpool

Etihad Stadium
Manchester, England
Saturday, 1 April 2023
Kick-off is at 14h30  
 
Manchester City inatarajia kupiga jeki azma yake ya kutwaa ubingwa wa ligi ya Premier watakapoalika Liverpool ugani Etihad Stadium Jumamosi Aprili mosi. 
 
The Citizens walishuhudia wapinzani wao wa karibu Arsenal wakipanua nafasi baina yao hadi alama 8 baada ya kuibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Crystal Palace kabla ya ligi kuchukua mapumziko mnamo Machi 19 huku vijana wa Pep wakishiriki mechi ya kombe la FA wikendi hiyo. 
 
City walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya the Eagles ugani Selhurst Park hapo awali ikiwa ni ushindi wa tatu mfululizo na kufikisha msururu wa mechi sita bila ksuhindwa katika ligi. 
 
Matumaini ya Manchester United kushinda taji la premier yalionekana kuyeyuka waliposhindwa 7-0 na Liverpool ugani Anfield kabla ya kwenda sare na Southampton uwanjani Old Trafford.
 
The Red Devils wapo katika nafasi ya 3, alama 11 nyuma ya City walio na mchezo mmoja mkononi huku Liverpool wakishika nafasi ya sita kwenye jedwali. 

Kevin De Bruyne
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Vijana wa Jurgen Klopp walipoteza 1-0 dhidi ya Bournemouth ugani Vitality Stadium Machi 11 katika mechi iliyofuata ushindi dhidi ya Machester United. 
 
Kwa sasa Liverpool wapo katika nafasi ya 6 na alama 42 baada ya kupoteza mechi ya nane ya msimu iliyovunja msururu wa mechi tano bila kushindwa, sawia na Brighton na Brentford wanaoshika nafasi ya 7 na 8 mtawalia wakiwa na alama 42. 
 
Kevin De Bruyne amekuwa na mchango mkubwa katika juhudi za City kutetea taji la premier msimu huu huku akichangia kupatikana magoli 13 kwenye mechi 25. Hata hivyo raia huyo wa Ubelgiji hajafikisha idadi ya magoli (15) aliyokuwa nayo msimu uliopita ila amefikisha na kuzidi idadi (8) ya magoli aliyochangia msimu uliopita. 
 
Ilimchukua muda Cody Gakpo kuzoea ligi ya Premier ila sasa makali yake yameanza kuonekana. Mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka PSV Eindhoven mwezi Januari hakufunga goli hata moja katika mechi tatu za kwanza lakini alifanikiwa kufunga magoli manne kwenye mechi sita zilizofuata ikiwa ni pamoja na magoli mawili dhidi ya United.

Cody Gakpo
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwenye habari ya vikosi, wenyeji watakosa mchezaji Phil Foden ambaye alifanyiwa upasuaji wikendi iliyopita. Erling Haaland anauguza jeraha la kinena na inawezekana asishiriki mechi hiyo. Calvin Ramsay (goti) na Stefan Bajcetic (kinena) wanauguza majeraha ya muda mrefu na hawataweza kushiriki mechi hiyo kwa faida ya Liverpool. Majeruhi wengine wa Liverpool ni pamoja na Thiago Alcantara (kinena), Luis Diaz (goti), Joe Gomez na Darwin Nunez.
 
Mafanikio ya City msimu huu yatategemea pakubwa na matokeo yao mwezi Aprili kulingana na meneja Guardiola huku wakifukuzia ubingwa katika mashindano matatu. 
 
"Ni kweli. Matokeo ya Aprili yatachangia pakubwa mafanikio yetu msimu huu. Tulifanya vizuri sana mwezi Februari na Machi. Mwezi Aprili ukiwa mzuri basi tutahitaji kufanya vizuri zaidi mwezi Mei,” alisema raia huyo wa Uhispania. 
 
"Kuwa kwenye mashindano matatu; Premier League, FA Cup na UEFA kufikia mwezi Aprili ni dhihirisho tosha tumekuwa tukifanya vizuri. Hilo ni wazi.”
 
Klopp amesisitiza umuhimu wa kumalizia msimu kwa matokeo mazuri huku wakitafuta kumaliza katika nne bora mwishoni mwa msimu kwani watapata nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa ulaya. 
 
"Jukumu letu ni kujituma zaidi na kumaliza katika nafasi nzuri kulingana na uwezo wetu msimu huu,” alisema raia huyo wa Ujerumani. “Michezo yetu miwili ya mwisho na hasa dhidi ya Manchester United tulionyesha uwezo wa kucheza soka ya kuvutia. 
 
"Mechi dhidi ya Bournemouth ambayo ni timu yenye uwezo mkubwa pia hatukuonyesha kiwango kizuri. Hilo linaongeza shinikizo kwetu.
 
"Timu nyingine zilishinda mechi zao hivyo basi tunazidi kuwa nyuma zaidi. Lengo letu ni kumaliza nne bora.” 
 
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi. 
Mechi - 5
Man City - 1
Liverpool - 1
Sare - 3
 
Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 29:
 
Aprili 1 Jumamosi
 
2:30pm: Manchester City v Liverpool
 
5:00pm: Bournemouth v Fulham
 
5:00pm: Arsenal v Leeds United
 
5:00pm: Brighton & Hove Albion v Brentford
 
5:00pm: Crystal Palace v Leicester City
 
5:00pm: Nottingham Forest v Wolverhampton Wanderers
 
7:30pm: Chelsea v Aston Villa
 
Aprili 2 Jumapili
 
4:00pm: West Ham United v Southampton
 
6:30pm: Newcastle United v Manchester United
 
Aprili 3 Jumatatu
 
10:00pm: Everton v Tottenham Hotspur


Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 03/29/2023