Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 English Premier League
Matchday 26
Liverpool v Manchester United
Anfield
Liverpool, England
Sunday, 5 March 2023
Kick-off is at 18h30
Baada ya kushinda taji la kwanza chini ya Erik ten Hag, Manchester United wataelekeza nguvu zao kwenye
mechi ya ligi dhidi ya Liverpool ugani Anfield Jumapili Machi 5.
The Red Devils walikuwa na wiki ya kufana baada ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Newcastle Wembley Jumapili iliyopita na kunyanyua kombe la EFL. Awali ya ushindi huo, United waliibandua Barcelona kutoka ligi ya Europa na kuingia hatua ya 16 bora ya shindano hilo.
Vile vile, vijana wa Ten Hag wameonyesha nia yao kwenye ligi baada ya kushinda mechi saba kati ya kumi za mwisho za ligi na kupoteza mechi moja tu. Kwa sasa wapo katika nafasi ya tatu alama sita nyuma ya viongozi wa ligi Arsenal.
The Gunners wanazidi kuwa alama mbili mbele ya Manchester City waliopo katika nafasi ya baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Leicester Jumamosi iliyopita. Vile vile, Manchester City waliibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Bournemouth kuendeleza shinikizo dhidi ya Arsenal.
Tottenham wanashikilia nafasi ya nne, alama nne nyuma ya Manchester United baada ya kuwashinda Chelsea 2-0 Jumapili iliyopita licha ya kuwa wamecheza mchezo mmoja zaidi ya United.
The Reds waliendelea kuandikisha matokeo mseto baada ya kutoa sare ya 0-0 na Crystal Palace Jumamosi iliyopita na kuwaacha alama tisa chini ya nafasi ya nne. Kwa sasa wanashikilia nafasi saba.
Hata hivyo hakukuwa na mabadiliko makubwa kwenye jedwali katika timu zinazofukuzia kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya baada ya Fulham (6) na Wolves (9) kutoa sare huku Brighton (8) na Chelsea (10) kupoteza mechi zao.
Timu ya Jurgen Klopp ilishinda mechi mbili mfululizo, dhidi ya Everton na Newcastle baada ya mechi nne kwa mpigo bila ushindi kabla ya sare dhidi ya Palace.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Virgil van Dijk ameshiriki mechi mbili tu baada ya kuuguza jeraha la misuli ya paja lililomuweka nje na kupelekea kukosa mechi nne za ligi. Raia huyo wa Uholanzi atakuwa na kibarua cha kumdhibiti mshambuliaji Marcus Rashford anayetikisa nyavu kwa hiari. Van Dijk amekuwa na kiwango cha kutamausha msimu huu akiwa na Liverpool kwani safu yao ya ulinzi imekuwa ikiruhusu mabao kiholela.
Rashford amekuwa katika hali nzuri tangu aliporejea kutoka kombe la dunia akifanikiwa kufunga magoli 17 katika michezo 19 ya mashindano yote, magoli matano yakija katika mechi tano za mwisho za ligi. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaonekana kuwa na msimu mzuri akiwa na timu yake kwani amefunga magoli 25 katika mechi 38.
Kwenye vikosi, wenyeji wanazidi kukosa baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza huku Thiago Alcantara (kinena), Luis Diaz (goti), Joe Gomez (misuli), Ibrahima Konate (paja) na Darwin Nunez (bega) wakitarajiwa kukosa mechi dhidi ya United. Christian Eriksen (kisigino) na Anthony Martial (kinena) wa United watakosa mechi hiyo pamoja na mejeruhi wa muda mrefu remain Donny van de Beek (goti).
Klopp alisema kuwa anatazama sare dhidi ya the Eagles kuwa alama moja iliyopatikana na sio alama mbili zilizopotea huku akiwaasa wachezaji wake kutia bidii zaidi wakitazamia kuboresha msimu ambao tayari sio mzuri kwao.
"Sharti tuzidi kupambana. Tujifunze na kuendelea. Hilo ni lengo letu,” alisema raia huyo wa Ujerumani.
"Hakuna kikubwa kilichobadilika katika mchezo huu. Hatukushinda mchezo wa leo ila tumepata alama moja zaidi. Hilo linatia moyo.”
Ten Hag alimaliza kiu cha miaka sita bila taji Old Trafford kwa kushinda kombe la EFL na anaamini maamuzi yake kuifunza United yanazaa matunda.
"Pengine yalikuwa maamuzi magumu ila napenda changamoto. Naipenda United,” alisema raia huyo wa Uholanzi. “Nafurahi kuona jezi zetu, uhusiano wetu na mashabiki, nafurahi kuona Old Trafford na historia aliyoacha Sir Alex Ferguson.
"Wachezaji maarufu na mahiri walikuzwa kwenye timu za United na inavutia sana. Tunataka kuendeleza hilo.
"Timu hii inatamani kuandikisha historia yake. Nafasi hii ilipojitokeza nilifahamu hii ni klabu mwafaka kwangu. Nilitaka kuhushwa nayo.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Liverpool - 3
Man United - 1
Sare - 1
Ratiba ya mechi ya ligi ya Premier mchezo wa 26:
Machi 4 Jumamosi
2:30pm: Manchester City v Newcastle United
5:00pm: Arsenal v Bournemouth
5:00pm: Aston Villa v Crystal Palace
5:00pm: Brighton & Hove Albion v West Ham United
5:00pm: Chelsea v Leeds United
5:00pm: Wolverhampton Wanderers v Tottenham Hotspur
7:30pm: Southampton v Leicester City
Machi 5 Jumapili
4:00pm: Nottingham Forest v Everton
6:30pm: Liverpool v Manchester United
Machi 6 Jumatatu
10:00pm: Brentford v Fulham
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.