EPL: Fulham v Arsenal


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 27

Fulham v Arsenal

Craven Cottage
London, England
Sunday, 12 March 2023
Kick-off is at 16h00  
 
Arsenal watakuwa wageni wa Fulham kwenye mechi ya ligi ugani Craven Cottage mnamo Jumapili Machi 12.  
 
The Gunners walilazimika kutoa jasho zaidi kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya Bournemouth Jumamosi iliyopita walipotoka nyuma magoli mawili na kushinda mechi hiyo dakika ya 97 kupitia goli la Reiss Nelson.
 
Ushindi wa nne mfululizo kwa Arsenal umeendelea kuwapa uongozi kwenye ligi, alama tano juu ya nafasi ya pili Manchester City walioshinda Newcastle United 2-0 mapema siku hiyo.
 
Timu mbili zinaonekana kung’anga’nia taji la ligi hasa baada ya Manchester United kupata kipigo kikubwa cha 7-0 mikononi mwa Liverpool Jumapili iliyopita na sasa wapo alama 14 nyuma ya viongozi wa ligi huku wakiwa na mechi moja mkononi.
 
Tottenham wanashikilia nafasi ya nne, alama nne nyuma ya the Red Devils baada ya kupoteza 1-0 dhidi ya Wolves nao Liverpool wakakwea hadi nafasi ya tano baada kushinda mechi ya nne katika mechi tano za ligi zilizopita.

Aleksandar Mitrovic
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
The Cottagers ambao ni Fulham wapo nyuma ya Liverpool na alama tatu kuelekea mchezo wao na Brentford Jumatatu Machi 6 huku Marco Silva akitarajia kufikisha msururu wa mechi tano bila kushindwa baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Wolves hivi majuzi.
 
Brighton wanaoshikilia nafasi ya 8 walishinda West Ham 4-0 Jumamosi iliyopita na sasa wapo alama moja nyuma ya Fulham ambao wapo mbele ya wapinzani wao wajao Brentford  kwa alama nne.
 
Aleksandar Mitrovic amekuwa na ushawishi mkubwa kwa Fulham msimu huu huku akifanikiwa kufunga magoli 11 kwenye mechi 19. Raia huyo wa Serbia alisaidia Fulham kupandishwa daraja msimu 2021-22 huku akifunga magoli 43 katika mechi 44 waliposhinda taji la daraja la pili.
 
Thomas Partey alishiriki mechi ya kwanza dhidi ya Bournemouth baada ya kuwa nje kwa mechi tatu kutokana na jeraha. Mchezaji huyo wa Ghana amekuwa kiungo muhimu kwa timu ya Arsenal na alifunga goli lake la tatu la msimu kwenye ushindi dhidi ya Bournemouth.

Thomas Partey
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwenye habari ya vikosi, Joao Palhinha anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi moja baada ya kupata kadi 10 za njano na anaungana na Tom Cairney (jeraha la kisigino), Neeskens Kebano (mguu) na Layvin Kurzawa (goti) ambao watakosa mechi hiyo. Arsenal watakosa huduma za Eddie Nketiah (kisigino), Leandro Trossard (kinena), Gabriel Jesus na Mohamed Elneny (wanauguza jeraha la goti).
 
Kiungo wa Fulham Andreas Pereira amewaasa wachezaji wenzake kujituma zaidi baada ya kukosa ushindi wa tatu mfululizo mikononi mwa Wolves.
 
"Hutukufurahia matokeo kwenye mechi dhidi ya Wolves ila tuna nafasi ya kuonyesha uwezo wetu,” alisema raia huyo wa Brazil.
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Fulham - 0
Arsenal - 4
Sare - 1
 

Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 27.

 
Machi 11 Jumamosi
 
3:30pm: Bournemouth v Liverpool
 
6:00pm: Everton v Brentford
 
6:00pm: Leeds United v Brighton & Hove Albion
 
6:00pm: Leicester City v Chelsea
 
6:00pm: Tottenham Hotspur v Nottingham Forest
 
8:30pm: Crystal Palace v Manchester City
 
Machi 12 Jumapili
 
5:00pm: Fulham v Arsenal
 
5:00pm: Manchester United v Southampton
 
5:00pm: West Ham United v Aston Villa
 
7:30pm: Newcastle United v Wolverhampton Wanderers
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 
 

Published: 03/10/2023