Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 English Premier League
Matchday 28
Chelsea v Everton
Stamford Bridge
London, England
Saturday, 18 March 2023
Kick-off is at 20h30
Chelsea watakuwa wenyeji wa Everton ugani Stamford Bridge Jumamosi Machi 18 katika
mechi ya ligi huku wakifukuzia ushindi wa tatu mfululizo kwenye shindano hilo.
The Blues waliibuka na ushindi wa 3-1 ugenini dhidi ya Leicester uwanjani King Power Jumamosi iliyopita na kuandikisha ushindi wa pili mfululizo tangu Graham Potter kutwaa mikoba Stamford Bridge kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Crystal Palace Oktoba 1 2022.
Ushindi wa 1-0 dhidi ya Leeds Machi 4 ulivunja msururu wa mechi tano bila ushindi kwa Chelsea ambao wapo katika nafasi ya kumi alama mbili juu ya Aston Villa.
Chelsea wapo alama moja nyuma ya Brentford wanaoshikilia nafasi ya tisa na alama saba nyuma ya Newcastle walio katika nafasi ya tano huku mbio kuingia katika nne bora zikipamba moto.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
The Toffees walipata afueni kwa ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Brentford Jumamosi iliyopita na kukatisha msururu wa mechi tatu bila ushindi na kuimarisha nafasi yao kusalia katika ligi.
Everton chini ya Sean Dyche imepoteza mechi tatu tu kati ya mechi saba za ligi zilizopita tangu aliporithi mikoba kutoka kwa Framk Lampard Januari 30 na ushindi dhidi ya Brentford uliwapandisha hadi nafasi ya 15 kwenye jedwali.
Timu hiyo kutoka Merseyside ipo alama moja nyuma ya Nottingham Forest walio katika nafasi ya 14 na alama mbili nyuma ya Wolves (13) na Palace (12) baada ya timu zote tatu kupoteza mechi zao wikendi iliyopita.
Hatimaye Kai Havertz alipata bao baada ya mechi sita bila kufunga goli alipofungia Chelsea bao la pili dhidi ya Leicester. Lilikuwa ni goli la sita kwa Mjerumani huyo msimu huu na anabakisha magoli mawili tu kusawazisha idadi yake ya msimu uliopita.
Dwight McNeil alifunga goli lake la kwanza chini ya mkufunzi Dyche ambaye alikuwa mwalimu wake kwa miaka minne akichezea Burnley. Mchezaji huyo wa miaka 23 aliaminika sana na Dyche ugani Turf Moor na sasa ameweza kucheza katika mechi zote saba tangu walipoungana tena na meneja wake wa zamani.
Kwenye vikosi, Potter atawakosa wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza kama vile Armando Broja, Thiago Silva (goti), Cesar Azpilicueta (kichwa), Edouard Mendy (kiganja), Mason Mount (kinena) na N'Golo Kante (paja). Kuna uwezekano Reece James ambaye ni mgonjwa, Raheem Sterling (paja) na Pierre-Emerick Aubameyang (mgongo) hawatashiriki mechi hiyo. Andros Townsend (goti) na Dominic Calvert-Lewin (paja) watakosa mechi hiyo kwa faida ya wageni.
Potter ameshuhudia uuwiano kwenye kikosi chake baada ya wiki ya matokeo mazuri ambapo walishinda mechi mbili za ligi na mechi moja ya UEFA dhidi ya Borussia Dortmund.
"Limekuwa ni juma lenye mafanikio. Tumefanikiwa kushinda mechi tatu. Tulianza vizuri dhidi ya Leeds, kisha dhidi ya Dortimund na pia ushindi wa leo. Ni ishara nzuri kutoka kwa wachezaji hawa kwa sababu sio jambo rahisi katika ligi ya premier,” alisema.
"Tumeonyesha juhudi kubwa na umoja kama kikosi wiki hii. Inachukua muda kulete uuwiano huu lakini tunazidi kuukuza. Napata furaha kuona tukikua. Kuna juhudi za pamoja na wachezaji wanajituma na wapo tayari kupambania timu.”
Dyche ana imani timu yake ipo kwenye mkondo mzuri baada ya kupata alama 10 kutokana na mechi saba alizokuwa na timu hii.
"Timu hii inazidi kuonyesha ukakamavu. Mtazamo wao umebadilika. Wakati mwingine unacheza dhidi ya timu ambayo haijapoteza mechi hata moja katika mechi 12. Mchezo tulioonyesha ulistahili alama zote tatu,” alisema.
"Inachukua muda kuafikia malengo yetu ila kuna ishara nzuri. Wanafanya mazoezi yanayostahili kuwapa nguvu.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Chelsea - 2
Everton - 2
Sare - 1
Ratiba ya mechi za premier mchezo wa 28:
Machi 17 Ijumaa
11:00pm: Newcastle United v Nottingham Forest
Machi 18 Jumamosi
6:00pm: Aston Villa v Bournemouth
6:00pm: Brentford v Leicester City
6:00pm: Southampton v Tottenham Hotspur
6:00pm: Wolverhampton Wanderers v Leeds United
8:30pm: Chelsea v Everton
Machi 5 Jumapili
5:00pm: Arsenal v Crystal Palace
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.