Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 English Premier League
Matchday 31
Liverpool v Watford
Anfield
Liverpool, England
Saturday, 2 April 2022
Kick-off is at 14h30
Liverpool watakuwa na nafasi ya kuongoza jedwali la
ligi ya Premier watakapoialika Watford ugani Anfield Jumamosi Aprili 2 katika mechi ya ligi.
The Reds wamekuwa wakiziba pengo kati yao na Manchester City kila uchao na ushindi wa 2-0 dhidi ya Arsenal ulipunguza tofauti baina yao na City kuwa alama.
Liverpool wamekuwa wakionyesha makali yao na sasa wamecheza mechi 10 bila kushindwa, ikijumuisha ushindi wa mechi tisa mfululizo.
Mwezi Aprili una ratiba ngumu kwa Liverpool kwani watakuwa na mechi za ligi dhidi ya Manchester City, Manchester United na Everton na vile vile Benfica katika mechi ya ligi ya UEFA.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk anasema kuwa ni wakati ratiba ngumu lakini wako tayari baada ya kushinda kombe la EFL na sasa wanafukuzia mataji mengine matatu.
"Ni kitu ambacho kila mchezaji anakitamani. Ni muhimu kujiweka vizuri kiafya kuhakikisha unafanya maandalizi ya mechi vizuri,” Van Dijk alizungumza na tovuti ya klabu.
"Jambo la kwanza muhimu ni kufurahia unapocheza. Usisahahu hilo. Kwa mfano leo, ni matokeo ya kufurahia ambapo unapigania kila taji. Aprili tunatakiwa kufanya vivyo hivyo.”
Kwa upande mwingine, The Hornets walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Southampton katika mechi waliyocheza ya mwisho ya ligi, na kuwapa nafuu kubwa katika vita vya kuepuka kushushwa daraja, na sasa wapo katika nafasi ya 18.
Ushindi huo ulikatisha msururu wa mechi nne bila kushinda kwa vijana wa Roy Hodgson, ambao walikuwa wamefungwa magoli saba katika mechi mbili za awali; Arsenal (3-2) na Wolves (4-0).
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Hodgson alisifia safu yake ya ulinzi kwa kustahimili mashambulizi ya dakika za mwisho kutoka kwa Southampton, na kuwaonya kuwa watarajie hali kama hiyo katika mechi tisa zilizosalia.
"Ustahimilivi ni muhimu sana katika mechi za ligi ya Premier,” alisema. “Haijalishi kama upo chini au nafasi za juu katika jedwali. Ni sharti uwe na uwezo wa kuzuia mipira yote inayoelekezwa kwenye himaya yako. Haya yote yanahitaji ustahimilivu ili kufaulu.
"Mechi nyingi kuelekea ukingoni zitakuwa hati hati dakika za mwisho. Wapinzani watakuwa wakishambulia sana lango lenu. Huwezi kuepuka kadri uhitajiwa wa kusalia katika ligi unapokuwa mkubwa. Ni ushindi mkubwa na utachochea uchu wa kushinda mechi za nyumbani na ugenini vile vile.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi
Mechi - 5
Liverpool - 4
Watford - 1
Sare - 0
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.