Spurs na Hammers kupigania nafasi ya nne


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021/22 English Premier League

Matchday 30

Tottenham Hotspur v West Ham United

Tottenham Hotspur Stadium
London, England
Sunday, 20 March 2022
Kick-off is at 19h30  
 
Tottenham watakuwa na kibarua cha kuongeza matumaini yao kumaliza katika nafasi nne bora watakapoalika West Ham United ugani Tottenham Hotspur Stadium Jumapili Machi 20.
 
Jumamosi iliyopita, vijana wa Antonio Conte walipoteza 3-2 dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford na kutia dosari mpango wao wa kumaliza nne bora
 
Spurs ambao wapo katika nafasi ya nane kwenye ligi walikuwa wameshinda mechi mbili za awali kwa mabao mingi; Leeds (4-0) na Everton (5-0) ingawa wana mechi tatu mkononi dhidi ya timu tatu zilizopo mbele yao.
 
Arsenal ambao wanachukua nafasi ya nne katika jedwali la ligi wamewaacha Spurs kwa alama sita huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.


Antonio-Conte-inter-milan-manager.jpg
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Kabla ya kuivaa West Ham United wikendi inayokuja, Tottenham watakuwa mgeni wa Brighton siku ya Jumanne na Conte amekiri kuwa wachezaji wake wanafaa kujiandaa kwa ratiba ngumu wiki hii.
 
"Tuna mechi mbili ngumu. Dhidi ya Brighton ambao walikuwa na mchezo mzuri dhidi ya Liverpool na mchezo dhidi ya West Ham United ambao pia wanapigania nafasi ya nne,” Conte aliiambia Spurs TV.
 
"Tutapumzika kidogo na kujiandaa kucheza siku ya Jumanne na tena siku ya Jumapili.”
 
West Ham waliimarisha nafasi yao kumaliza nne bora baada ya kuishinda Aston Villa 2-1 ugani London Stadium Jumapili iliyopita.
 
Timu ya David Moyes ilikuwa imepoteza mechi dhidi ya Liverpool 1-0 wiki moja awali, na kukatisha msururu wa mechi nne bila kushindwa. Kwa sasa wapo nafasi ya sita, alama tatu nyuma ya Arsenal huku wakiwa na mechi tatu zaidi.  

David-Moyes.jpg
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Moyes amefurahishwa na uchezaji wa timu yake kwa ujumla na mafanikio waliyopata msimu huu na ana imani wataendelea hivyo hivyo ili kupambana na timu kubwa.
 
"Nimefurahishwa sana na wachezaji wangu tangu msimu ulipoanza na jinsi wanavyojituma,” alisema Moyes. “Huu ndio mwanzo tu katika safari ya kupambana na timu kubwa.
 
"Aston Villa wametumia fedha nyingi na wametengeneza kikosi kizuri kilicho na wachezaji wazuri. Kwetu sisi, tunapambana kadri ya uwezo wetu na tulichojaliwa na tutaendelea kupambana na kujiimarisha.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 zilizopita za ligi.

Mechi - 5
Tottenham - 2
West Ham - 2
Sare - 1

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 03/18/2022