Roma na Lazio katika debi della Capitale


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021/22 Italian Serie A

Matchday 30

AS Roma v SS Lazio

Stadio Olimpico 
Rome, Italy 
Sunday, 20 March 2022 
Kick-off is at 20h00 
 
AS Roma watafufua uhasama na wapinzani wao wa jadi SS Lazio watakapokutana katika mechi ya ligi ugani Stadio Olimpico Machi 20.
 
Roma walipambana kupata sare ya 1-1 katika mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Udinese Calcio uliochezwa Machi 13.
 
Roma hawajashindwa katika michezo minane ya ligi iliyopita baada ya kuandikisha ushindi mara nne na kupata sare katika mechi nne.


Jose-Mourinho-Roma-manager.jpg
Hakimiliki ya picha: Getty Images 


Vile vile, Roma hawajashindwa katika mechi nne za ligi wakiwa nyumbani huku wakiandikisha sare mara mbili mfululizo na ushindi mara mbili ugani Stadio Olimpico.
 
"Ulikuwa mchezo mgumu. Nahisi iwapo tungesawazisha mapema tungekuwa na nafasi ya kufukuzia goli la ushindi,” alisema meneja wa Roma Jose Mourinho baada ya sare hiyo dhidi ya Udinese.
 
"Bahati mbaya tulisawazisha dakika za mwisho. Sasa ni mechi nane bila kushindwa katika ligi; ushindi mara nne na sare nne. Ukitazama sare tulizopata nyumbani, unaweza kusema tulipoteza alama mbili.
 
"Unaposawazisha mechi katika dakika za mwisho kabisa angalau unakuwa hujashindwa.”


Maurizio Sarri
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Kwengineko, Lazio waliishinda Cagliari Calcio 3-0 katika mechi iliyopita ya ligi ya tarehe 5 na watakuwa wenyeji wa Venezia Machi 14.
 
Awali kabla ya ushindi dhidi ya Cagliari, Lazio walikuwa wameshindwa mechi moja na kupata sare moja kwenye mechi mbili zilizopita.
 
Hata hivyo, Lazio hawajashindwa katika mechi nne za ligi wakiwa ugenini baada ya kuandikisha sare moja na ushindi mara tatu.
 
Mechi ya ligi ya mwisho baina ya timu hizi ilikuwa mnamo Septemba 26 2021.
 
Lazio waliibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Roma katika mechi iliyoandaliwa ugani Stadio Olimpico, uwanja ambao unatumiwa na timu hizo mbili
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi

Mechi - 5
Roma - 1
Lazio - 2
Sare - 2


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 03/17/2022