Quartararo anatazamia ushindi wa kwanza Indonesian Grand Prix


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2022 MotoGP Season

Indonesian Grand Prix

Round 2
Mandalika International Street Circuit
Central Lombok, Indonesia 
Sunday, 20 March 2022

Fabian Quartararo anatazamia kupata ushindi wa kwanza katika mbio za pikipiki za msimu wa 2022 MotoGP wa Indonesian Grand Prix Machi 20.
 
Mwendeshaji huyo kutoka Ufaransa alianza kutetea taji lake la MotoGP kwa kumaliza katika nafasi ya tisa kwenye mbio za Qatar Grand Prix mnamo Machi 6.
 
Quartararo alikuwa katika nafasi ya 11 kwenye mkondo mwanzoni mwa mbio kabla ya kupitwa na Johann Zarco wa Pramac kwa sekunde 0.007 na kuchukua nafasi ya nane.


Enea Bastianini
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Mwendeshaji wa pikipiki wa kampuni ya Ducati Enea Bastianini alishinda mbio za Qatar 2022 huku nafasi ya pili ikitwaliwa na Brad Binder wa kampuni ya KTM.
 
Nafasi ya tatu ilitwaliwa na mwendeshaji wa kampuni ya Honda Pol Espargaró katika mbio hizo zilizoandaliwa kwenye mkondo wa Losail International Circuit, Losail.
 
Kwa hivyo, Muitaliano Bastianini anaongoza katika jedwali la waendeshaji pikipiki huku akifuatiwa na Binder na Espargaro mtawalia.
 
Kwa sasa, Quartararo anashikilia nafasi ya tisa katika jedwali la waendeshaji akiwa na alama saba. Iwapo atashinda mbio za Indonesia basi ataimarisha nafasi yake kwenye jedwali.


Brad Binder
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
“Ukizingatia tulishinda mbio zote mbili mwaka jana na sasa tunamaliza katika nafasi za nyuma zaidi, ndio kuna wasiwasi,” alisema Quartararo baada ya mbio za Qatar 2022.
 
“Siwezi kusema kuwa najiamini sana kuelekea Qatar. Lakini, Kama ninavyopenda kusema, mimi sio mhandisi.
 
“Kazi yangu ni kupambana asilimia mia moja katika kila mbio na hali yoyote. Iwapo napigania ushindi basi nitaweka juhudi asilimia mia moja,” aliongeza mwendeshaji huyo mwenye umri wa miaka 22.
 
“Kwa vyovyote vile nitapambana kadri ya uwezo wangu bila kujali nafasi niliyopo.”
 
Kampuni ya Ducati inaongoza katika jedwali la wazalishaji, ikifuatiwa na KTM na kisha Honda mtawalia.
 

Matokeo ya Qatar Grand Prix 2022

Mshindi: Enea Bastianini - Ducati
Nafasi ya pili: Brad Binder - KTM
Nafasi ya tatu: Pol Espargaró - Honda


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway. 
 
 

Published: 03/18/2022