Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 MotoGP World Championship
2022 Qatar Grand Prix
Losail International Circuit
Lusail, Qatar
Sunday, 6 March 2022
Bingwa mtetezi wa dunia wa Yamaha Fabio Quartararo anatarajia kushinda Qatar Grand Prix kwa mara ya kwanza mashindano ya 2022 MotoGP yatakapong’oa nanga Jumapili Machi 6.
Mfaransa huyo alishinda taji lake la kwanza la
MotoGP mwaka 2021 baada ya kumaliza alama 26 mbele ya Francesco Bagnaia wa Ducati kwenye msimamo wa waendeshaji piki piki.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
Quartararo alimaliza katika nafasi za jukwaani mara kumi msimu uliopita huku akiibuka na ushindi mara tano kati ya nafasi hizo ambazo ni; Doha Grand Prix, the Portuguese Grand Prix, the Italian Grand Prix, the Dutch TT na the British Grand Prix.
Hata hivyo, dereva huyo mwenye umri wa miaka 22 hajashinda katika mkondo wa Losail International Circuit huku akimaliza katika nafasi ya tano katika mbio zilizopita na 16 katika mbio za 2019.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
Quartararo alikiri kuwa katika mazoezi ya kabla ya msimu kuanza huko Mandalika, aliifanyisha mazoezi pikipiki yake ya mwaka 2022 lakini hakupata matokeo aliyokuwa akitarajia.
“Asubui ya leo nilienda kasi sana lakini sikujihisi vizuri. Sijafurahi,” aliiambia Autosport. “Mazingira yalikuwa yale tu mchana wa leo. Nilifurahi kwa sababu zaidi ya muda wa mzunguko mmoja, nilijihisi vizuri.
"Tulifika mwisho wake na nilihisi hivyo kila mahali. Muda niliotumia kwenye mzunguko mmoja uliimarika lakini nilitarajia ungekuwa mzuri zaidi. Qatar itakuwa ni hali tofauti. Niko asilimia mia moja tayari.”
Matokeo ya 2021 Qatar Grand Prix
Mshindi: Maverick Vinales - Yamaha
Nafasi ya pili: Johann Zarco - Ducati
Nafasi ya tatu: Francesco Bagnaia - Ducati
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni
soka,
motorsport,
mpira wa kikapu,
rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.