Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Italian Serie A
Matchday 29
AC Milan v Empoli FC
Stadio Giuseppe Meazza
Milano, Italy
Saturday, 12 March 2022
Kick-off is at 22h45
AC Milan watapambana na Empoli FC katika
mechi ya ligi ugani Stadio Giuseppe Meazza mnamo Machi 12.
Rossoneri SSC waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya SSC Napoli wakiwa ugenini katika mechi ya ligi iliyopita ya tarehe 6 Machi.
Kwa sasa, Milan hawajashindwa katika mechi sita za ligi zilizopita huku wakiandikisha sare tat una kushinda mechi tatu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Vile vile, Rossoneri hawajashindwa mechi yoyote kati ya mechi tatu zilizopita wakiwa nyumbani huku wakishinda mechi moja na kupata sare mbili Stadio Giuseppe Meazza.
“Ni alama tatu muhimu hasa kwa sababu tulishinda timu kubwa. Haya yalikuwa ni matunda ya kujituma sana kwa wachezaji wetu,” alisema meneja wa Milan, Stefano Pioli baada ya ushindi dhidi ya Napoli.
“Ulikuwa ni mchezo mgumu hasa walipokuwa wanatushambulia. Walimdhibiti Osimhen kwa weledi mkubwa. Kazi yetu baada ya kupoteza mpira ilikuwa nzuri.
"Tumeridhishwa sana. Ni alama moja zaidi tu wakati huu ukilinganisha na msimu jana. Kuna kazi zaidi ya kufanya. Mpango mkubwa ni kujiimarisha.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Empoli walilazimisha sare ya 0-0 dhidi ya Genoa ugenini katika mechi iliyopita ya ligi iliyochezwa tarehe 6 Machi.
Inamaanishwa kuwa, Empoli hawajashinda mchezo wowote wa ligi katika michezo kumi na moja iliyopita, huku wakishindwa mara tano na kwenda sare katika mechi sita.
Vile Vile, Empoli hawajashinda mechi yoyote katika mechi sita wakiwa ugenini. Wameshindwa mechi moja na kupata sare tano.
Mchezo wa mwisho baina ya Milan na Empoli katika ligi ulikuwa Disemba 22 2021.
Mila waliishinda Empoli 4-2 kwenye mechi iliyochezewa Stadio Carlo Castellani, ambao umechukua jina la mchezaji wa zamani wa Empoli Carlo Castellani.
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 zilizopita za ligi
Mechi - 5
Milan - 3
Empoli - 1
Sare - 1
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.