Hakimiliki ya picha: Getty Images
Philadelphia 76ers v Dallas Mavericks
2021-22 NBA Regular Season
Saturday 19 March 2022
Wells Fargo Center, Philadelphia, Pennsylvania
Tip-off at 02:00
The Dallas Mavericks wanapania kuendeleza msururu wa matokeo mazuri ya msimu huu wa
NBA watakapokutana na Philadelphia 76ers katika ukumbi wa Wells Fargo Center huko Philadelphia, jimbo la Pennsylvania asubuhi ya Jumamosi Machi 19.
The Mavericks wanachukua nafasi ya tano Western Conference wakiwa na rekodi ya 42-26 na wanaifukuzia Utah Jazz kumaliza katika nafasi ya nne baada ya kushinda mechi nane kati ya kumi za mwisho.
Vijana wa Jason Kidd waliishinda Boston Celtics 95-92 Jumatatu huku Luka Doncic akifunga vikaku 26 kwa faida ya wageni, na kocha wa Mavericks amemsifia sana mchezaji huyo.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Ni mchezaji mwenye maarifa sana. Anatambua vitu vingi na sio uwanjani tu, bali hata kwenye kanda na mikutano,” alisema Kidd. “Anafuatilia kila jambo kwa kina. Ana uwezo mkubwa kiakili na wengi wengi wameshuhudia hilo.”
The 76ers wapo katika nafasi nzuri ya kumaliza kwenye nafasi za kucheza mechi za mchujo japokuwa matokeo ya hivi karibuni yamekuwa sio mazuri sana.
Joel Embiid na James Harden walichangia alama 34 na 24 mtawalia dhidi ya Denver Nuggets Jumanne lakini haikutosha kwani walipoteza mechi hiyo 114-110 wakiwa nyumbani.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Embiid anaongoza kwenye chati za ufungaji katika ligi msimu huu na anatarajiwa kushinda taji la mchezaji bora wa msimu baada ya kukosa taji hilo mwaka 2021. Nikola Jokic alishinda taji la mwaka 2021 huku akiwa amecheza mechi 21 zaidi.
"Nafikiri Joel anataka kucheza zaidi na alisema hivyo mwaka uliopita,” alisema kocha wa 76ers Doc Rivers. “Alisema, “Nataka kuwa katika hali nzuri kimazoezi. Nahitaji kucheza mechi zaidi ili kuisaidia timu yangu.” Nafurahi sana kwa sababu anacheza sana.”
The Mavericks walishinda 107-98 wakiwa ugenini dhidi ya 76ers katika mchezo uliopita wa Februari 4, huku Doncic akichangia pakubwa sana katika mchezo huo.
Takwimu baina ya Philadelphia 76ers dhidi ya Dallas Mavericks, NBA
Mechi: 80
76ers: 39
Mavericks: 41
Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.