Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 Corales Puntacana Championship
US PGA Tour
Puntacana Resort and Club
Punta Cana, La Altagracia, Dominican Republic
24-27 March 2022
Mashindano ya golfu ya
Corales Puntacana Championship ya 2022 yamepangiwa kuchezewa Cana, La Altagracia, Jamhuri ya Dominika kati ya tarehe 24 na 27 Machi.
Baada ya kuasisiwa mwaka 2016 kama shindano la Web.com Tour, shindano hili lilipandishwa na kuwa PGA Tour kuanzia mwaka Machi 2018.
Ni shindano la kwanza la PGA Tour kuandaliwa katika Jamhuri ya Dominika na zawadi yake ni sawa na mashindano mbadala lakini bado halijapata mwaliko kushiriki Masters.
Joel Dahmen ndiye bingwa mtetezi wa taji la Corales Puntacana Championship baada ya kushinda shindano la mwaka jana.
Mashindano ya mwaka huu yatajumuisha wachezaji kama; Jimmy Walker, Danny Willett, Bill Haas, Nick Taylor, Tyler Duncan, Sung Kang, Martin Trainer na wengineo.
Shindano litakuwa na wachezaji 120 na linatazamiwa kuchezwa kwa muda wa siku nne huku likiwa ni shindano la 23 katika ratiba ya msimu wa 2021-22 wa PGA Tour.
Washindi wa zamani wa shindano hili la Corales Puntacana Championship Brice Garnett, Nate Lashley, Graeme McDowell na Hudson Swafford watakuwa miongoni mwa washiriki wa mwaka huu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“PGA Tour na wanachama wet una washiriki wengine wanafurahi kurudi Puntacana Resort & Club," alisema Tyler Dennis, Rais na makamu mtendaji wa PGA TOUR.
"Baada ya kuandaliwa kwa ufasaha, Korn Ferry Tour ilipandishwa na kuwa shindano la PGA Tour mwaka 2018.
"Shindano hili limezidi kukua na kuimarika na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii,” alisema.
"Tunatazamia miaka zaidi ya mashindano makubwa na kuzidi kuitangaza Jamhuri ya Dominika kwa mashabiki wetu kote duniani.”
Washindi 5 wa mwisho wa Corales Puntacana Championship
2017 - Nate Lashley - Marekani
2018 - Brice Garnett - Marekani
2019 - Graeme McDowell - Northern Ireland
2020 - Hudson Swafford - Marekani
2021 - Joel Dahmen - Marekani
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.