Mallorca kukabana koo na Madrid


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Spanish La Liga

Matchday 28

Real Mallorca v Real Madrid

Visit Iberostar Estadi
Palma de Mallorca, Spain
Monday, 14 March 2022
Kick-off is at 23h00  
 
Real Mallorca watakuwa mwenyeji wa Real Madrid katika mchezo wa ligi ugani Iberostar Estadi Machi 14.
 
The Vermillions walipoteza 4-3 mechi dhidi Celta Vigo ugenini katika mchezo wa ligi uliochezwa Machi 6.
 
Mallorca hawajashinda mechi ya ligi katika mechi nne zilizopita, huku wakipoteza mechi zote nne mfululizo.

Luis Garcia Plaza
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Vile vile, Mallorca hawajashinda mechi yoyote katika mechi mbili zilizopita wakiwa nyumbani baada ya kushindwa katika mechi zote mbili.
 
Kwengineko, Real Madrid waliishinda Real Sociedad 4-1 wakiwa nyumbani katika mechi iliyochezwa mnamo Machi 5.
 
Kwa sasa, Madrid hawajashindwa katika mechi saba za ligi huku wakiandikisha ushindi mara tano na kupata sare mbili.
 
Madrid wameandikisha ushindi mara moja na kupata sare moja katika mechi mbili za ligi zilizopita wakiwa ugenini.

Carlo Ancelotti
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Tulikuwa na mchezo mzuri kuanzia dakika ya kwanza. Mpango wetu ulikuwa kuwashinikiza ili kuowaondoa katika mbinu yao ya kuanza mchezo kutoka nyuma,” alisema Carlo Ancelotti baada ya ushindi huo.
 
"Ulikuwa mchezo mgumu lakini tuliumudu. Ulikuwa mchezo wenye maana kubwa kwa sababu ulitupa nafasi ya kuendeleza uongozi wetu katika jedwali la ligi.
 
"Tulicheza kwa furaha na wachezaji walielewa umuhimu wa mechi hii. Huu ndio mchezo mashabiki wetu wanapenda kushuhudia na wanatusaidia kufanya vizuri. Ni imani yangu tutaendelea hivyo hivyo.”
 
Mchezo wa mwisho baina ya timu hizi mbili katika ligi ulikuwa Septemba 22 2021.
 
Madrid walionyesha mchezo mzuri na kushinda kwa mabao 6-1 katika mechi iliyochezewa ugani Visit Mallorca Estadi ambao kwa sasa ulijulikana kama Iberostar Estadi hapo awali. 
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi

 
Mechi - 5
Mallorca - 0
Madrid - 5
Sare - 0


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 03/08/2022