Madrid wapania kisasi dhid PSG


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 UEFA Champions League 

Round of 16 - Second-Leg

Real Madrid v Paris Saint Germain (PSG)

Estadio Santiago Bernabéu
Madrid, Spain 
Wednesday, 9 March 2022
Kick-Off 23h00  
 
Real Madrid wataalika Paris Saint Germain (PSG) katika mechi ya ligi ya UEFA hatua ya 16 bora mkondo wa pili mnamo Mchi 9.
 
Miamba hao wa soka kutoka Uhispania walishindwa mechi ya mkondo wa kwanza 1-0 wakiwa ugenini Parc des Princes Februari 15.
 
Matokeo hayo yalifikisha kikomo msururu wa Madrid wa mechi nne za shindano hili bila kushindwa, baada ya kuandikisha ushindi mara nne mfululizo.

Toni Kroos
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Madrid hawajashindwa katika mechi mbili zilizopita za shindano hili wakiwa nyumbani huku wakiandikisha ushindi katika mechi zote.
 
 
Kwingineko, PSG wana imani watapata ushindi katika mechi ya marudiano dhidi ya Madrid, ambayo ni timu yenye mafanikio makubwa katika historia ya mashindano haya. Mechi hiyo itachezawa ugani Estadio Santiago Bernabéu.
 
PSG imeshinda mechi mbili za mwisho mfululizo za shindano hili.
 
Hata hivyo, PSG hawajashinda mechi yoyote katika mechi nne zilizopita za mashindano haya wakiwa ugenini huku wakiandikisha sare mbili na kushindwa katika mechi mbili.

Kylian Mbappe
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Tumepata kuwasoma wapinzani wetu japokuwa sio sana kwa sababu utakuwa ni mchezo tofauti kabisa,” alisema mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe baada ya kufunga goli la pekee dhidi ya Madrid.
 
"Muktadha wa mechi utakuwa tofauti na mechi itakuwa tofauti kabisa. Tumejiandaa kwa ajili ya mechi kama hizi kwa sababu ni ndoto kushiriki.
 
"Tulihitaji kushinda na mashabiki wetu walitushabikia. Tunafurahi kwa ushindi huo lakini bado kuna mechi ya marudiano na mechi za ligi zinazokuja kabla ya wakati huo.”
 
Mara ya mwisho Madrid kuwaalika PSG katika mechi ya UEFA ilikuwa Novemba 26 2019.
 
Mchezo huo uliishia sare ya 2-2 ugani Estadio Santiago Bernabéu
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mechi za UEFA

 
Mechi - 7
Madrid - 3
PSG - 2
Sare - 2

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 03/08/2022